Halloween party ideas 2015
Image



RAIS MAGUFULI  IPA SHAVU NEC


Na Yusuph Mwamba


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, ameipongeza tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), kwa kusimamia zoezi la Uchaguzi vizuri na kuahidi kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo kuwa na jengo lao binafsi.
Rais Magufuli akipokea hundi ya pesa kutoka kwa Mwenyekiti wa NEC, Lubuva iliyobaki kwenye bajeti ya uchaguzi mkuu wa Tanzania 2015 hafla hiyo iliyfanyika Ikulu Dar es salaam


Akizungumza na waandishi wa habari,  Jijini Dar es Salaam, wakati akikabidhiwa ripoti ya Uchaguzi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Rais Magufuli amesema kuwa atatoa shilingi bilioni 12 kwa ajili ya ujenzi wa majengo hayo ambapo amependekeza ujenzi wa majengo hayo ufanyike Mkoani Dododoma.

Mwenekiti wa NEC, Lubuva akiteta jambo na Rais Magufuli Ikulu Dar es salaam kabla ya kuelekea kupewa kiasi walicho rudisha kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la ofisi yao iliyopendekezwa ijengwe Dodoma.

Rais  Magufuli amesema kuwa,  kulingana na jitihada kubwa ilizozionesha tume hiyo, licha ya kukabiliwa upungufu wa bajeti wa kununua vifaa vya uandikishaji huku kukiwa na ufinyu wa maadalizi lakini waliweza kufanikisha kuandikisha kwa wakati zoezi la zima la  uchaguzi wa upigaji kura Nchi nzima.



Aidha Rais Magufuli, amesema kuwa miongoni mwa changamoto zinazoikabili taasisi  ya uchaguzi (NEC) ni pamoja na  Tume kutokuwa na ofisi yake yenyewe kutokana na ufinyu wa kazi zake tume haitawiki kukaa katika jengo la kupanga,hivyo ameamua kurudisha bajeti ya tume iliyobaki ambayo Mwenyekiti wa NEC ariirudisha kwa Rais, na Rais kuwarudishia tume hiyo ili iweze kujenga majengo ya Tume.

Aidha, Rais Magufuli ameitaka tume hiyo ya NEC kuwa licha ya zoezi hilo kukamilika ,lakini tume inahitaji kuendelea na shughuli zake za kawaida ikiwemo kuboresha daftari la kudumu la wipiga kura pamoja na utoaji wa elimu ya mpiga kura na kusimamia chaguzi ndogondogo.


Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.