Halloween party ideas 2015
Image





SERIKALI YA TANGAZA HALI YA HATARI' ATAKAYE OA NA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI KIFUNGO MIAKA 30 JELA


Na Yusuph Mwamba

SERIKALI imewasilisha  bungeni hoja ya  Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ya Mwaka 2016, unaokusudia pamoja na mambo mengine, kutoa adhabu ya miaka 30 jela kwa mtu yeyote atakayeoa au kuolewa na mwanafunzi wa shule ya msingi au ya sekondari.
Adhabu hiyo iko katika marekebisho yanayokusudiwa kufanywa katika Sheria ya Elimu Kifungu cha 60, kinachokusudiwa kufanyiwa marekebisho kwa kuongezewa vifungu vinavyopiga marufuku ndoa kwa wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari.
Kifungu cha 60 (a), kifungu kidogo cha kwanza, ambacho ndio kipya kimeeleza kuwa itakuwa kinyume cha sheria katika mazingira yoyote yale kwa mtu yeyote kumuoa au kuolewa na mwanafunzi wa shule ya sekondari au ya msingi.
Kwa mujibu wa kifungu hicho kipya, mtu yeyote atakayekiuka kifungu hicho, sheria hiyo imeweka wazi kuwa atakuwa ametenda kosa na adhabu yake itakuwa kufungwa jela miaka 30.

Sehemu ya tatu ya sheria hiyo,imeeleza wazi kuwa mtu yeyote atakayempa mimba mwanafunzi wa shule ya msingi au wa shule ya sekondari, atakuwa ametenda kosa, ambalo adhabu yake pia ni kwenda jela miaka 30.

Baadhi ya Watoto Bungeni wakisikiliza hoja mbalimbali za wabunge Dodoma.

Sheria hiyo imekwenda mbali zaidi kwa watu watakaokutwa na hatia ya kushawishi mwanafunzi wa shule ya msingi na shule ya sekondarin aoe au aolewe, wakati akiendelea na shule, naye atakuwa amefanya kosa na adhabu yake ni faini isiyopungua Sh milioni tano, au kwenda jela miaka mitano au vyote kwa pamoja.

Ili kudhibiti hali hiyo, sheria hiyo imewataka wakuu wa shule na walimu wakuu waliyoko kila pembe ya Tanzania yani Bara na Visiwani kutunza  kumbu kumbu na taarifa juu ya wanafunzi wao na kuziwakilisha kwa kamishna wa serikali au mwakilishi wake itakayoeleza kwa kina matukio ya ndoa na mimba za wanafunzi na hatua zilizochukuliwa za kisheria dhidi ya waliokutwa na hatia.

Marekebisho hayo ya sheria ya elimu, yamewasilishwa bungeni wiki hii, wakati Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA) likiitaja Tanzania kuwa moja ya nchi tatu zinazoongoza kwa ndoa za utotoni.

 

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.