Na Yusuph Mwamba
KLABU ya Soka ya Tottenham, wamefanikiwa kubomoa safu ya kiungo ya klabu ya Southampton baada ya kumsainisha Mwanandinga wa Kimataifa wa Kenya , anayekipiga kunako klabu ya Southampton, Victor Wanyama kwa kandarasi ya miaka 5 hadi mwaka 2021.
Wanyama akiwa White Heart baada ya utambulisho wa kuitumikia klabu yake mpya Tottenham msimu ujao |
Wanyama mwenye umri wa miaka 24, aliyesajiliwa kunako klabu ya Tottenham, pia ameshawahi kuvitumikia baadhi ya vilabu mbalimbali ikiwemo klabu ya Celtic ya Scotland pamoja na klabu yake ya sasa Southampton.
Licha ya kuwaniwa na vilabu mbali mbali Barani Ulaya, klabu ya Manchester United ilishawahi kuiwinda saini ya kiungo huyo lakini dili la uhamisho lilishindikana na Mwanandinga huyo kubakia kunako klabu yake ya Thousampton.
Kiwango kizuzuri kilicho oneshwa na Nyota huyo, ndicho kilicho mvutia na kumfanya kocha Pochettino kutaka huduma ya mwandinga huyo.Huu ni usajili wa pili kwa Pochettino kuitaka saini ya mwanadinga huyo, baada ya kufanya kipindi anaitumikia klabu ya Soutrhampton alifanya usajili wa Wanyama akitokea kunako klabu ya Celtic mwaka 2013.
Kocha mkuu wa kikosi cha Tottenham Mauricio Pochettino |
" Nashukuru kwa sapoti kubwa iliyooneshwa na mashabiki wa klabu yangu ya Southampton tangu nitue hapa nikitokea klabu ya Celtic, nawapongeza pia viongozi wangu kwa ushirikiano mzuri waliouonesha juu yangu, lakini soka ni ajira acha niende nikatafute ajira sehemu nyingine asanteni sana naimani tupo pamoja pia muendelee kunitia moyo huko niendako naifanikiwe na kutimiza malengo yangu.". Alisema Wanyama
Wanya akijaribu kumtoka mchezaji wa Tottenham kwenye moja ya mchezo wa ligi kuu Uingereza EPL msimu wa mwaka 2015/2016 |
Post a Comment