Zikiwa zimepita siku chache tangu kuanza kwa tetesi za usajili Bara, tayari klabu ya Simba wameanza kunukia neema baada ya kuzagaa kwa taarifa za ujio wa aliyekua kocha wa zamani wa klabu ya Azam FC, Joseph Omong kutua kunako klabu hiyo ya Msimbazi bila ya ukakika wa kulamba dili la kuinoa klabu hiyo.
Tangu kumalizika kwa ligi kuu bara msimu wa 2015/2016, wekundu wa Msimbazi walionekana kuwa na mapungufu kadhaa huku wakihitaji nyota kadhaa kwa ajili ya kuimarisha na kujenga kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao wa wa ikiwemo ligi kuu bara ambapo kwa muda mrefu wekundu hao walikua wakiukosa na kutawaliwa na watani wao Yanga, lakini kubwa lililo zagaa maeneo ya Msimbazi ni kuhusu ujio wa Joseph Omong.
Akizungumzia kuhusu nani anafaa kuwa kocha wa klabu hiyo, mwanachama mmoja kutoka tawi la Simba Mpira pesa Ustadhi Masoud, ameseme kuwa soka la sasa haliangalii kocha anatoka nchi gani, ila muhimu ni uwezo wake wa kufundisha na timu ikapata mafanikio.
“Ujio wa makocha wa kuinoa Simba, viongozi walishapendekeza walimu wa klabu hiyo, lakini kubwa kwetu sisi tunaona jiana la Joseph Omong ndilo linalekodi nzuri ya mafaniko".Alisema Masoud
Ikimbukwe kuwa tangu mchakato wa mkusaka makocha wa kuifundisha klabu hiyo, mpaka sasa tayari Simba walishafanya mazungumzo na baadhi ya makocha ikiwemo Sellas Teteh ,Kalisto Pasuwa, na Omong ili kuangalia uwezekano wa kujiunga na klabu hiyo msimu ujao wa 2016/2017.
Masoud alisema uwezo wa Omong ni kielelezo tosha kwamba anaweza kufundisha Simba kwa mafanikio kulinganisha wengine.
Wakati huo Mosoud akizungumza hayo,pia Mwenyekiti wa Tawi la Vuvuzera, Paul Makoye, alisema jana kuwa uongozi wa klabu ya Simba upo makini na tayari walishaangalia rekodi za makocha wote na kugundua kuwa kulingana na ubora wa Omong ni dhahiri anafaa kukabidhiwa timu na kurithi mikoba ya Mayanja aliyeipokea timu katikati ya msimu wa 2015/2016.
Moja ya rekodi aliyowahi kuandika kocha huyo wa zamani wa Azam FC, Joseh Omong, ni kufutia kuiwezesha klabu ya AC Leopards ya Congo Brazavile kutwaa kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2012.
Post a Comment