PUMA YAFUNGUKA, YATOA MAJIBU BAADA YA KASHFA YA UTENGENEZAJI JEZI FAKE
Na Yusuph Mwamba
ZIKIWA zimepita siku chache baada ya shutuma ya Kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo kwa ubora Duniani Puma, kutokuwa na ubora juu ya bidhaa zake, Mwanandinga wa kimataifa wa Uswis, Xherdan Shaqiri, alikaririwa akisema kapuni hiyo haina uwezo wa kutengeneza kondom baada ya mchezo wao dhidi ya Ufaransa kufuatia kuchanika kwa jezi za wachezaji wanne wa timu hiyo ya Uswis.
Kampuni hiyo yenye makao makuu yake Nchini Ujerumani, ilipata tuhuma hizo kwenye mchezo wa fainali ya Euro 2016 kati ya timu ya Taifa ya Ufaransa wenyeji wa mashindano hayo dhidi ya timu ya Taifa ya Uswia baada ya ya jezi za Wanandinga wa Uswizi ,Breel Embolo, Granit Xhaka, Admir Mehmedi na Blerim Dzemaili kuchanika katika mchezo uliomalizika kwa amokeo a 0-0.
Licha ya mamalalamiko hayo kutolewa na mwanandinga huyo, pia Nyota wa zamani wa Gary Lineker, aliandika kwenye mtandao wake wa jamii wa Twitter akidiliki kukashifu bidhaa hizo za kampuni ya Puma kwa kusema “ Hata ukiangalia Jezi zao pamoja na mipira yao bado unatilia shaka juu ya ubora wa bidhaa yao na kushindwa kuweka dhamana bidhaa zinazozalishwa na kampuni hiyo maarufu Duniani kwa vifaa vya michezo, hapa naona Puma wanaanza kujipotezea ubora wao!”
Akizungumza na vyombo vya habari kufuatia kashfa hiyo kubwa, Mkuu wa kitengo cha habari wa kampuni ya Puma, Kerstin Neuber, amesema tukio hilo ni lakwanza na wala halijawahi kujitokeza.
“Hili ni tukio la kwanza kwa upande wa kampuni yetu ya Puma, hata ukiangalia mechi tano zilizopita mbona hakujawa na tukio hili? Waataamu wetu wa masuala ya utengenezaji wa vifaa vyetu wapo makini sana katika kufanyia uchunguzi Material ya jezi zetu na endapo yatatokea matatizo na kuyatambua mapema tutatoa taarifa rasmi". Alisema Neuber
Moja ya wachuuzi wa jezi za Puma nchini Uswizi Ramon Serrano amesema: “Ilionekana dhahiri kwamba sehemu ya namba katika jezi ilikuwa imejichora sana kiasi ya kuwa hatarini kuchanika.
Nyota wa Uswis Xhaka, akinyosha kidole kwa mwamuzi kuashilia kuchanika kwa jezi yake katika fainali ya michuano ya Euro2016 kati ya Uswis dhidi ya Ufaransa. |
Post a Comment