Na Yusuph Mwamba
KLABU ya Simba imekamilisha dili la usajili wa kiungo mchezeshaji, Mohammed Ibrahim( Rasta) ,kwa kandarasi ya miaka miwili kutoka klabu ya mtibwa Sugar tayari kukitumikia kikosi hicho msimu ujao 2016/2017.
Akizungumza na waandishi wa Habari mkuu wa kitengo cha habari wa klabu hiyo, Haji Manara, amethibitisha kuwepo kwa usajili huo na kusema kwamba umezingatia nmatakwa ya benchi zima la ufundi chini ya kocha Mayanja.
Moja ya makubaliano ya Rasta na Simba ni kulipwa kiasi cha shilingi 250,000 kwa kila mchezo Simba inaposhinda yeye akiwa kikosini lakini dau lake la usajili limefichwa kutokana na sababu maalumu.
Mpaka sasa klabu hiyo ya Msimbazi imefanikiwa kunasa saini za wanandinga wanne, miongoni mwa wanandinga haoni ni Mohamed Ibrahim (Rasta) , Muzamir Yassin wote kutoka Mtibwa Sugar, Jamal Mnyate na Emmanuel Semwanza wote wakitokea klabu ya Mwadui FC iliyoko Shinyanga.
Licha ya kuwasajili nyota hao, Simba bado inaendelea kufanya mazungumzo ya usajili na wachezaji wengine akiwemo kiungo wa Mtibwa, Shiza Kichuya.
|
Mohamed Ibrahim ( Rasta) akijaribu kumtoka mlinzi katika moja ya mechi ya VPL 2015/2016 |
Post a Comment