Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba 

MAKAMU wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, amekemea vikali baadhi ya tabia chafu zinazofanywa na wana vyuo wa kike hapa Nchini wanaodiriki kushirki kuuza mili yao katika hoteli na makumbi makubwa ya starehe na kuwataka kucha tabia hiyo kwani ipo nje na maadili yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa Habari, Makamu wa Rais ,Mama Samia  Suluhu,kwenye viwanja vya Chuo hicho Kikuu ya katika hafla ya  kuadhimisha siku ya wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe pamoja na Uzinduzi wa kampeni za uchangiaji wa Ujenzi wa Bweni la wanachuo wa kike ,amesema kamwe hafurahishiwi na viitendo hivyo na kusema vinavunja maadili ya Nchi yetu na Kupelekea kupungua kwa nguvu kazi hapa Nchini na hatimaye kubeba maradhi.
Aidha, Makamu wa Rais Mama Samia,Alisema baadhi ya wanafunzi hao walidiriki kujiuza miili yao kwa ajili ya tamaa ya kupata vitu vya anasa zikiwemo simu zenye gharama kubwa, mavazi na vitu vingine jambo ambalo linafedhehesha jamii, wazazi na walezi wenu.
Makamu wa Rais, alitumia fursa hiyo kuwataka wanafunzi wa kike wanaosoma katika vyuo vikuu Nchini kujikita zaidi katika elimu ili waweze kufanikiwa kujikwamua kiuchumi  kwenye maisha yao ya baadaye na familia zao.
“Vyuo siku hizi vimeharibika kwa tamaa, sisi tulisoma hapa Mzumbe na tuliweza kuishi na kuendana na mazingira, lakini wanafunzi wa sasa  wengi wenu mnaingiwa na tamaa ya mashindano ya mavazi utadhani mnagombea Umiss” Alisema Mama Samia.
Aliongeza kuwa, “nimeambiwa hapa Morogoro wapo baadhi ya wanachuo wa kike wanakwenda kujiuza miili katika hoteli moja kubwa na kwenye majumba ya starehe kwa tamaa tu, mnataka kuwa na simu ya laki saba na mavazi ya gharama kubwa itawezekana wapi, mnatukwaza wazazi wenu.” Aliongeza Mama Samia
Mama Samia akipitia Hotuba yake katika maadhimisho hayo viwanja vya maeneo ya Mzumbe University 
Makamu wa Rais Samia akijaribu kutoa ufafanuzi wa hotuba yakekatika hafla hiyo Chuo kikuu cha Mzumbe
Makamu wa Rais  Samia akiwaasa wanafunzi wa kike juu ya kufuata maadili mema









Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.