Halloween party ideas 2015
Image


TIMUA TIMUA YA VIGOGO WENYE MADENI NYUMBA ZA SERIKALI YAANZA RASMI LEO. 

Na Yusuph Mwamba

VIGOGO wakiwamo wabunge na wananchi wengine, walionunua nyumba za serikali na kutomaliza kulipa madeni yao kwa wakati kama mikataba yao inavyoelekeza, wameanza kuondolewa kwa nguvu kwenye nyumba hizo na nyumba kupigwa mnada ili kupata fedha za kulipa madeni ya Sh bilioni sita ambayo serikali inadai kupitia Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

 Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Yono Auction Mart ambayo ilipewa mamlaka na kazi ya kuhakikisha inakusanya mara moja madeni hayo ya TBA kutoka kwa wadaiwa sugu ambao hawataki kulipa madeni na badala yake kutaka kuishi kwa mteremko wa Serikali, Scholastica Kevela, alisema kuwa kazi ya kuwaondoa vigogo walionunua nyumba hizo au kupangisha bila kulipa, inaanza rasmi leo jijini Dar es Salaam.

Moja ya Nyumba zinazodaiwa kukaliwa na Vigogo bila malipo ya kodi

Kevela, alisema katika kazi hiyo, TBA wamewapa orodha ya zaidi ya nyumba 3,000 Nchi  mzima za walionunua na wengine kupangisha nyumba za TBA ambao wanadaiwa madeni na muda wao wa  kurejesha ulishapita tangu waanze kutumia nyumba hizo.

“Tuna jumla ya orodha ya nyumba 3,000 Nchi nzima ambazo zinadaiwa kodi , juzi tulianzia mkoa wa  Mwanza na tukafanikiwa kushikilia zaidi ya  Nyumba 20, kwa kuwatoa watu nje, halikadhalika na Dodoma pia  tulifanya hivyo, mpaka sasa tumefanikiwa kushikilia nyumba 40 zikiwemo za vigogo, kesho (leo), tunaanza zoezi hilo hapa Dar, hatutakuwa na na mzaha kwa mdaiwa yeyote yule kwa vile wote tulishawapatia  taarifa za kimaandishi mapema ili kuwa muda wa kujiandaa, kazi yetu ni utekelezaji tu” Alisema Kevela.

Aidha, amesisitia kuwa wanatekeleza kazi waliyopewa kwa sababu hata ,Rais John Magufuli, anasisitiza wananchi kulipa kodikwa maendeleo ya Taifa  na kuacha utegemezi wa misaada ya kimashariti toka Nchi zilizo endelea, hivyo wadaiwa sugu hao muda wa kulipa na hata muda wa ziada waliopewa kuhakikisha wamemaliza madeni yao nao ulipita na wengi hawakulipa, hivyo basi Yono inaingia kazini kupiga mnada nyumba hizo kutekeleza agizo walilopewa.

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.