Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba

MAKAMU  Mwenyeketi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa ,Philip Mangula, amewaangukia wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani  na kuwaomba warudi bungeni, kwani michango yao  katika bunge la Jamhuri ya Mungano inaumuhimu mkubwa hasa ukizingatia katika kipindi hiki kigumu cha uchangiaji  katika  Bunge la Bajeti.
Mangula, amezungumza hayo baada ya  kufuatia  hatua ya wabunge wa kambi rasmi ya Upinzani wanaounda umoja wa UKAWA ,kususia vikao vinavyoendeshwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dk. Tulia Ackson, ikiwa ni  kwa kile kinachodaiwa kutokuwa na imani naye.Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mangula alisema michango ya wapinzani ina umuhimu mkubwa na pia ni wachangiaji wazuri bungeni.

Michango ya wabunge wa upinzani ina umuhimu mkubwa hasa katika mijadala ya kupitisha bajeti ya Nchi, ambayo pia inagusa katika majimbo yao, sasa basi kutoka nje ya Bunge si njia pekee ya kutatua matatizo kwa kuwa ndani ya vikao hivyo ndipo zinapojadiliwa changamoto mbalimbali za majimbo yao ambayo yote yanategemea Bajeti kuu, ni vema warudi hatua stahiki zitachukuliwa kufanya hivyo wanawanyima haki waliowachagua".Alisema Mangula


Aidha, alisisitizia suala la kususia vikao na kwenda kuijadili bajeti nje ya Bunge hakutaweza kuleta manufaa kwa Taifa na hata kwenye majimbo yao na baadala yake warudi Bungeni kuendelea na masuala ya kitaifa yanayoendelea hivi sasa.

Akizungumzia suala la adhabu walizopewa wabunge saba  wa upinzani, Mangula alisema kila jambo lina utaratibu na kanuni zake za kufuata kwahiyo kwa Mbunge yeyote atakaye kwenda kinyume na maadili ya Bunge na kutofuata kanuni na sheria adhabu lazima imwangukie haijalishi Upinzani wala chama tawala kincoangaliwa ni haki kwa wa Wabunge wote wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Makamu mwenyekiti CCM Taifa Phillip Mangula akifafanua jambo juu ya Wapinzani kugomea Bajeti

















Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.