Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba

HATIMAYE Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  limepiga kura na kupitisha bajeti  kuu ya serikali yenye jumla ya shilingi Trilioni 29.5 kwa mwaka wa fedha 2016/17 licha ya wabunge wa kambi ya upinzani kutoka nje ya ukumbi wa bunge wakiwa wamebandika karatasi kuziba midomo yao kwa kile kinachodaiwa kunyimwa uhuru ndani ya Bunge hilo.Zimepita takribani siku 23, tangu Mei 30 mwaka huu ambapo wabunge wa kambi rasmi ya upinzani na wanaounda Ukawa wamesusie kushiriki katika vikao vya bunge ambapo Juni 20 ikiwa ni siku ya kuhitimisha mjadala wa bajeti kuu ya Serikali, wabunge hao wameamua kuziba midomo kwa gundi na karatasi na kutoka nje ya ukumbi wakilalamikia uendeshaji na bunge hilo kutokuwa na haki na usawa.

Akijibu hoja ya bunge kuwa Raba Stempu, mwanasheria mkuu wa serikali ,George Maseju ,amepinga vikali hoja ya bunge kuwa Raba Stempu, amesema chombo kinachoendeshwa kwa majadiliano kwahiyo kinahitaji umhimu mkubwa  wa kuzingatia katiba na sheria na kusema kwambakwa ni kiunganishi cha wananchi na serikali yao.

Akijibu hoja za wabunge ,waziri wa fedha na uchumi,Dr Phillip Mpango ,amesema serikali haitaongeza tozo ya kodi katika mafuta na itajielekeza katika kuimarisha miundombinu ya miradi.

Aidha, amesisitiza kuwa serikali imeondoa msamaha wa kodi kwa mafao ya viongozi wa kisiasa, na kusisitiza kuanzia sasa kiinua mgongo cha wabunge, mawaziri, rais, wakuu wa mikoa na wilaya vitatozwa kodi ili kujenga misingi ya usawa na haki kwa ajili ya maendeleo ya Taifa letu kwa ujumla.
James Mbatia akiwa na wabunge wa upinzani leo nje ya bunge wakiendeleza mgomo wao 

Waziri wa fedha Dr Philip Mipango akionyesha bajeti ya fedha ya Serikali ya Tanzania Bungeni









Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.