UCHAGUZI MKUU WA KLABU HIYO.
Na Yusuph Mwamba
KATIKA mchakato wa luelekea kwenye uchaguzi mkuu wa klabu ya Simba SC, tayari baadhi ya matawi yameshaanza mchakto wa vikao kujadili mambo yanayoihusu klabu yao ya Msimbazi ambayo kwa muda mrefu imeonekana kutofanya vizuri katika ligi kuu ya Tanzania Bara kwa misimu minne mfululizo.
Tawi la Simba la Kinondoni, ni miongoni mwa tawi ambalo limeanza mchakato huo katika kuelezea matakwa yao kama wanchama ili kuisaidia klabu hiyo ya Msimbazi kuweza kufanya vizuri katka michuano mbalimbali msimu ujao ikiwemo ligi kuu ya Tanzania Bara ambayo kwa muda mrefu, Simba imekua ikishiriki pasipo na mafanikio ma kuambulia nafasi ya tatu. huku ikiwaacha watani zake Yanga ikitawala soka la Tanzania licha ya Azam kuonesha upinzani.
Akiuzungumza na waandishi wa habari, mwenyekiti wa matawi Wilaya ya Kinondoni, Omary Maslahi, amesema lengo la kufanya kikao hiko ni kutaka kuwasilisha mapendekezo na hoja zao kwa klabu na kuangalia wapi wamekosea na kujipanga tena katika msimu ujao ili waweze kuibuka mabingwa na kuwakilisha Nchi Kimataifa kama ilivyo kwa watani wao Yanga SC.
"| Kikao chetu kililenga zaidi kujipanga na msimu ujao 2016/2017 na kuangalia ni wapi wana Msimbazi tulikosea ili tujikite zaidi na kuibuka mabingwa wa ligi kuu ambapo ni muda mrefu takribani miaka minne hatujafanikiwa kuchukua ubingwa huo na kuhakikisha tunawakilisha Nchi kimataifa kam ilivyo kwa mahasimu wetu Yanga na ndio maana umeona kikao chetu kimehudhuriwa na Rais wetu wa klabu Eveva".Alisema Omary
Kuhusu hoja nya Makamu mwenyeki wa klabu hiyo Kaburu, baadhi ya wanasimba hao wamesema hawamwamini makau huyo kwani ni mnazi wa Yanga na kipindi yupo chuo UDSM 1991-1993alishawahi kuwa mwenyekitiwa tawi la Yanga chuoni hapo huku James Mbatia akiwa mwenyekiti wa tawi la Simba chuoni hapo.
Kikao hicho kilicho fanyika mwishoni mwa juma lililopita juni 19, 2016 maeneo ya Ngawaiya, Manzese Argentina, pia kilihudhuriwa na Rais wa klabu ya Simba, Evans Eveva pamoja na Uongozi wake wa chini akiwemo msemaji wa klabu hiyo Manara, na klabu hiyo imepanga kufanya mkutano wake mkuu Julai 10, 2016 siku ya Jumapili ambako ukumbi wa mkutano huo utatajwa na msemaji wa klabu watakapo kuwa wamekubaliana na Uongozi wa klabu hiyo yenye makao yake makuu Kariakoo maeneo ya Msimbazi.
Baadhi ya wanachama wa Simba wakiwa katika mkutano huo wakimsikiliza Rais Eveva akinena jambo |
Uongozi wa Simba ukiongozwa na Rais Eveva katika mkutno wa wanacha wa klabu hiyo ulifanyika kinondoni |
Post a Comment