POLISI Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imesema bado inaendelea na msako wakumtafuta Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, kwa ajili ya mahojiano juu ya mahubiri yake aliyoyatoa wiki moja iliyopita yakiwa yanadaiwa kulenga uchochezi.
Akizungumza na waandishi wa habari, kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema jeshi hilo bado lina
endelea na msako wake wa kumtafuta Askofu huyo na kutoa ombi kwa yeyote atakaekuwa na taarifa juu ya aliupo Mchungaji huyo askofu huyo, asisite kupeleka taarifa Polisi ili akamatwe mara moja.
Kamanda Sirro alisema , Mpaka sasa hawajui Askofu Gwajima alipo lakini bado wanaendelea na msako kwa mahojiano zaidi.
“Tunaendelea kumtafuta, tunaamini tutampata ili ahojiwe, tunawaomba pia wananchi yeyote mwenye taarifa juu ya mahali alipo askofu huyo tunaomba watupe taarifa ili aweze kukamatwa” Alisema Sirro.
Askofu Gwajima anatafutwa na jeshi la polisi kwa kile kinachodaiwa juu ya mahubiri yake aliyoyatoa Juni 11,2016 mwaka huu kanisani kwake Ubungo Maji jijini Dar es Salaam.
Katika mahubiri hayo ambayo yalisambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, askofu huyo alisikika akiukosoa utendaji kazi wa Rais mstaafu Jakaya Kikwete aliyemaliza muda wake 2015 jambo ambalo linahatarisha maisha kwani kitendo cha kujaji mambo hayo ndin ya eneo la kusalia ni kinyume na sheria na pia linawagawa waamuni na kudai jambo hilo ni uchochezi wa amani.
Pia Gwajima alisikika akimshauri Rais John Magufuli, kuhama Chama Cha Mapinduzi (CCM) iwapo watakataa kumkabidhi uenyekiti wa chama hicho na kwamba apeleke muswada bungeni, kuondoa kinga ili rais ashtakiwe kwa makosa aliyoyafanya akiwa madarakani.
Post a Comment