![]() |
jicho la kushoto likiwa limejaribishiwa majimaji ya ngozi hiyo |
Huko marekani wanasayansi wamegundua ngozi yenye mithiri ya majimaji ambayo inafanya ngozi ya uzee kurudi ujana.
Ngozi hiyo ya majimaji ambayo bado yanafanyiwa majaribio kama bidhaa ya urembo katika maduka ya vipodozi yanatarajiwa kuuzwa kama dawa ya ngozi hapo baadae.
Ngozi hiyo ambayo inapakwa mwilini na kuachwa kukauka baadae huishia kuwa ngozi nyembamba inayofanana na ngozi ya ujana.
Aidha Kundi la wanasayansi kutoka chuo kikuu cha Havard kitengo cha matibabu na taasisi ya teknolojia Massachusetts wamefanya majaribio ya bidhaa hiyo kwa watu waliojitolea ambao walipakwa ngozi hiyo chini ya macho, kwenye mikoni yao na miguu.
Ngozi hiyo inayotokana na kemikali polysiloxane polymer iliundwa kwenye maabara kwa kutumia chembe chembe za Silicone na hewa safi ya Oxygen.
Licha ya kwamba sio ngozi ya kweli lakini imeundwa kuiga ngozi asili na pia kuacha nafasi ya hewa kupita.
Kwa mujibu wa watatfiti ngozi hiyo bandia ina uwezo wa kunasa mvuke na kusaidia ngozi kujivuta kiasi cha inavyostahili.
( bbc swahili)
Post a Comment