Ugonjwa ni jambo ambalo linawasumbua watu wengi sana na hupelekea kushuka kwa utendaji kazi wa shughuli za kujenga Taifa.
Kutokana na hali hiyo, kumekuwa na wimbi kubwa la wagonjwa wale wanao sumbuliw
a na magonjwa sugu pamoja na magonjwa ya mlipuko hivyo Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Mkuu wa mkoa kwa kushurikiana na baadhi ya vituo vya afya vimetenga siku 5 maalumu ambapo wakazi wote wa Dar e s salaam
watatakiwa kufika Mnazimmoja siku ya Jumatano Septemba 6 hadi septemba 10, asubuhi mpaka jioni kwa ajili ya kupima afya zao .
Akuzungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam ofisini kwake, Mkuu wa Mkoa, Poul Makonda, amesema lengo ni kuweza kubaini wagonjwa wanaosumbuliwa na maradhi sugu na wenye maraadhi ya mpito ili kupatiwa ufumbuzi kwa haraka bila malipo.
RC Makonda amesema kuwa , zoezi hili linalenga kuhamasisha wananchi kuwa na utamaduni wa kupima ili kujua afya zao ambapo kutawasaidia kuepusha gharama, na kuondokana na magonjwa na jinsi ya kuyaepuka baada ya kujua taarifa za ugonjwa.
Miongoni mwa magonjwa yatakayopimwa ni pamoja na kansa , tezi dume, macho, meno, na magonjwa mengineyo.
Aidha, Makonda amesema kutokana kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya ini , jopo la madaktari wanajipanga kuona ni kwa namna gani wanaweza kutatua kero hiyo kwa sababu ni ugonjwa hatari sana unoweza kupelekea kifo kwa haraka.
"Wakazi wa Dar e s salaam huu ndio wakati wenu najua miongoni mwetu fedha za kufanya vipimo vya afya ni tatizo lakini kwa kuwa karibu na wananchi wangu nimeona ni vyema tukakutana pamoja ili kujua afya zetu na wale watakao gundulika wana matatzio basi watapata maelezo ya kutosha kupitia kwa wataalamu wetu nataka kuona vifo vinasababishwa na Mungu sio kwa ugonjwa'', amesema RC Makonda
Mbali na Mkuu wa mkoa, naye Mganga mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Bi Grace Magembe amesema zoezi hilo litafanyika ndani ya siku tano kuanzia Jumatano mapaka jumapili.
Upimaji huo utakuwa ni bure bila tozo ya aina yeyote,ambapo wataalamu zaidi ya 200 watajitokeza katika utoaji huduma kwa wananchi.
''Nataka niwaweke wazi, katika zoezi la upimaji tutakuwa na mfumo mzuri wa kuwahudumia kwani tumepanga kila atakae fika atapatiwa huduma bila upendeleo na zoezi hili litakuwa ni la kila mwananchi baada ya kugundulika kuwa na matatizo, wagonjwa wote watahudumiwa na wale watakao stahili kupata rufaa atapewa kwa wakati unaotakiwa, tutawapatia rufaa na maelekezo wagonjwa wote kwa mgawanyo wa Hosptali kutokana na ukubwa wa tatizo na huduma zake''ameongeza Bi Grace
zoezi hili litashirikisha wadau kutoka serikalini na wengine kutoka taasisi binafsi ambapo kwa upande wa Serikali, madktari kutoka hospitai ya Taifa Muhimbili,jakaya Kikwete,Ocean Road,Amana ,Mwananyamala, Temeke, pamoja naTMJ,LEGENCY,AGAKHAN,IMILIFE,Chama cha watoa huduma binafsi,CCP MEDICINE,DAMU SALAMA,Shirikaa la MDH,Shirika la bima ya afya NHIF,KAIRUKI,SANITAS.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment