Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba
UMESIKIA HII!  kuwa mkoa wa Kilimanjaro upo hatarini kugeuka jangwa kutokana na kasi kubwa ya uvunaji wa miti unaofanywa na wananchi, ikiwa ni pamoja na kuendesha shughuli za kilimo na makazi karibu na vyanzo vya maji.
Kutokana na hatari hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki, ametoa agizo kwa wakuu wa wilaya pamoja na wakurugenzi mkoani hapa, kukagua vyanzo vyote vya maji na kuwachukulia hatua kali za kisheria wote wanaofanya kazi za kilimo na ujenzi wa makazi kandokando ya vyanzo hivyo vya maji.
Sadiki, ambaye awali alishawahi kuwa mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam kabla ya nafasi yake kuchukuliwa na Mh: Poul Makonda, alisema hayo wakati wa upandaji miti ulioandaliwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi (MUWSA), katika chanzo cha maji cha Shiri Njoro, kilichopo wilayani Hai mkoani hapa, ikiwa ni maadhimishio ya kukumbuka kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Upandaji miti huo pia unaelezwa kulenga kuenzi kujishughulisha kwa Hayati Mwalimu Nyerere, katika utunzaji wa mazingira.
Aidha Mh: Sadiki, Alisema kutokana na wananchi kuharibu mazingira kwa kiasi kikubwa, mji wa Moshi sasa umekuwa hatarini kugeuka jangwa, hali inayohatarisha uhai wa wananchi na uchumi wa taifa .
Licha ya kutoa agizo la kukamatwa, pia Mh: Sadiki ameitaka wizara husika baada ya  kusema kuwa kuna haja taasisi elekezi  zinazohusika na zoezi zima la uhifadhi wa vyanzo vyz maji pamoja na mazingira vitoe elimu ya kutosha kutokana na idadi kubwa ya wakazi hao kuitoielewa vizuri sera ya usafi pamoja na kuwa na elimu ndogo ya utunzaji na usafi wa Mazingira.
Sadiki alisema, miaka ya nyuma wananchi wa mkoa wa Kilimanjaro hawakuwa na tabia ya kugombea chanzo cha maji au maji ya umwagiliaji, lakini sasa watu wameanza kugombea maji kutokana na uhaba wa huduma hiyo iliyosababishwa na uvunaji wa miti kwa wingi.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Mjini Moshi (Muwsa), Joyce Msiru, alisema chanzo hicho kimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi katika kutoa huduma ya maji safi na salama, ambapo kimekuwa na uwezo wa kuzalisha mita za ujazo 12,000 kwa siku na kuhudumia zaidi ya wananchi 37,000 wa wilaya ya Hai na Manispaa ya Moshi.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline








Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.