Halloween party ideas 2015
Image

Na Issa Ramadhani
WAKALA wa Misitu Kanda ya Kusini wamemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dk Binilith Mahenge madawati 580 yenye thamani Sh milioni 43.

Madawati hayo yalikabidhiwa kwa mkuu wa mkoa na Kaimu Meneja wa Wakala wa Misitu Kanda ya Kusini, Vincent Embrantino Mgiye.
Mgiye alisema kwamba wakala huo umeitikia mwito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhakikisha kwamba wanafunzi wote wa shule za msingi na sekondari wanapata elimu kwa utulivu.
Akikabidhi madawati alisema kitendo hicho ni somo tosha kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ya kujua umuhimu wa misitu katika maendeleo yao leo na kesho.
Akipokea madawati hayo, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Dk Mahenge alisema ili kufikia uchumi wa kati, ni lazima kuimarisha miundombinu ya elimu ikiwa ni pamoja na kuboresha eneo la kusomea kuwa na walimu wenye wito, wazazi na serikali kushirikiana kulinda miradi ya elimu.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.