Halloween party ideas 2015
Image

Na Issa Ramadhani

UTUKUFU ni jambo la hekima kwa watu wenye roho ya kimumgu, lakini ndani ya roho hiyo ni lazima uwe mnyenyekevu katika kulitumikia dhehebu lako au dini yako, Hivyo ndivyo alivyofanya  Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis baada ya kumtunuku tuzo ya heshima ya mfano mwema Mtanzania, Janeth Mhella, kutokana na utumishi uliotukuka.

Mtanzania huyo, amekuwa Mwafrika wa kwanza kutunukiwa tuzo hiyo na Papa Francis, kutokana na  kumtumikia vyema kiongozi huyo na kanisa kupitia kazi aliyoifanya kwenye kituo cha redio.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana, ilieleza tuzo hiyo ya juu na ambayo mtu hawezi kuipata kwa urahisi ilitolewa Alhamisi iliyopita na Kiongozi wa Sekretarieti ya Mawasiliano ya Ofisi ya Papa, Monsinyori Dario Vigno. Pia, watumishi wengine watano walitunukiwa tuzo na sekretarieti hiyo.



Tuzo hiyo kwa Kiitaliano inaitwa ‘Pro Ecclesia et Pontifice’ yaani medali ya Latini na kwa Kiswahili fasaha ni medali ya kanisa na Papa. Tuzo hiyo ya Kanisa Katoliki ilianzishwa na Papa Leo wa 13 mwaka 1888.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.