Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba

KATIKA kitu kilichowashangaza wapenda soka wengi hapa nchini ni swala lililotoke juzi la Kariakoo Derby, baada ya washabiki wa Simba kung'oa Viti na kuvitupa uwanjani, Lakini  Serikali imetoa majibu na kuchukua uamuzi wa kuzuia fedha za mapato ya mechi kati ya Simba dhidi ya Yanga hadi hapo gharama za uharibifu wa viti katika mechi yao dhidi ya Yanga, itakapojulikana.

Akizungumza na waandishi wa habari Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye , amesema kwamba Simba inatakiwa kulipa gharama ya viti 1,781 vilivyoharibiwa na mashabiki wake.



Nape amesisitiza, fedha za mapato ya Simba zitaendelea kushikiliwa hadi hapo suala la gharama ya uharibifu itakapojulikana.

“Gharama ikijulikana, watakatwa mara moja. Na kama haitoshi, basi watalipishwa zaidi ,” Alisema Waziri Nape.

Pamoja na Nape kuzungumza adhabu juu ya kulipia gharama za uvunjwaji wa viti , serikali imetangaza kuzifungia Yanga na Simba kuutumia uwanja huo hadi hapo baadaye bodi itakapokaa na kukubaliana na Serikaili juu ya matumizi ya uwanja huo.

Mashabiki wa Simba waling’oa viti wakati wa mechi yao dhidi ya Yanga kwenye uwanja huo, juzi  ikiwa ni baada ya Amissi Tambwe kuifungia Yanga bao huku wakiamini bao lile halikuwa na uhalali .

Tambwe ambaye ni raia wa Burundi aliyetemwa na Simba kwa kile walichodai kushuka kwa kiwango , alifunga bao hilo baada ya kuunawa mpira, jambo ambalo lilisababisha tafrani hasa baada ya yeye kwenda kushangilia upande wa mashabiki wa Simba ikiwa ni moja ya kuwadhihaki na kuwaoneshea kuwa kwanini walimuacha.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.