Na Yusuph Mwamba
MATUMIZI ya dawa za kulevya kwa vijana limekuwa ni janga la Taifa, jambo ambalo limepelekea viongozi wa serikali kupambana kuhakikisha kuwa wanakabiliana na suala hilo ili kuweza kulinda nguvu kazi ya Taifa.
Kutokana na jambo hilo kuwa ni janga kwa Taifa letu, Mkuu Wa Wilaya ya Kigamboni Hashim Mgandilwa hivi karibuni alikutana na vijana walioacha kutumia madawa ya kulevya wanaoishi katika kituo cha Pedderef House of Wisdom, kilichopo Kigamboni ambao pia walishiriki katika Kampeni ya Mti Wangu iliyofanyika eneo la Daraja la Kigamboni kiwilaya.
Alipozungumza nao baada ya zoezi la Upandaji miti, DC Mgandilwa aliwapongeza kwa Uamuzi wao wa kuacha kutumia madawa ya kulevya.
Licha ya kutoa elimu kwa vijana juu ya kuacha kutumia madawa ya kulevya, lakini, DC Mgandilwa, aliwasihi kuendelea kujihusisha na shughuli mbalimbali za kijamii na kuwa wasirudie kutumia madawa ya kulevya kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha yao na bado jamii inawahitaji kwani ni nguvu kazi ya taifa.
DC Mgandilwa, alisema anafanya jitihada kubwa za kutambua maeneo ya vijana waathirika wa madawa ya kulevya wanakoishi na atashirikiana na hao walioamua kuacha ili kuwaelimisha vijana wenzao waachane na kutumia madawa ya kulevya na kujikita katika shughuli za kimaendeleo kama vile Ujasiriamali.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment