MENEJA wa klabu ya soka ya Chelsea, Antonio Conte, ameitaka klabu yake ya Chelsea wa cheze kwa juhudi kubwa kama wanahitaji mafanikio msimu huu wa 2016/2017.
Conte, ameyazungumza hayo mbele ya waandishi wa habari baada ya kutokuridhishwa na mfululizo wa mbaya wa matoko aliyoyapata licha ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya klabu ya Hull City.
Mpaka sasa klabu ya Chelsea, imeshacheza jumla ya michezo saba, imefanikiwa kushinda jumla ya michezo minne huku wakipoteza michezo miwili ambapo ilipokea kichapo kutoka kwa Liverpool 2-1 pamoja na klabu ya Arsenal 3-0 na kutoa sare mchezo mmoja.
Pamoja na matokeo hayo, Chelsea inashika nafasi ya saba baada ya kujikusanyia jumla ya alama 13 lakini matarajio ya kocha huyo ni kuwepo katika nafasi kubwa nne kitu ambacho kimeonekana kuwa na kikwazo katika safari yake.
"Ni kweli ligi imekuwa ngumu japo licha ya mategemeo niliyo yategemea baada ya kutua hapa lakini marekebisho yanatakiwa kufanyika katika idara ndogondogo naimani tutafanikiwa na tutakuwa na kiwango bora kama walichokionyesha mahasimu wetu Liver Pool, Arsenal, Manchester United pamoja na Manchester City kama tutashirikiana na kucheza kwa pamoja". Alisema Conte
Huku akianzia na marekebisho pamoja na kubadili mifumo mbalimbali, Conte amekuja na mfumo wa 3-4-3 ambapo aliutumia katika ushindi wa mabao 2-0 alioupata dhidi ya Hull City, lengo likiwa ni kupima uwezo wa mchezaji mmoja mmoja na kuangalia ni mchezaji gani atakae endana na mfumo wake ili kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya kupigania taji hilo linaloonekana kuwa gumu kutokana na timu zote kujipanga vizuri msimu huu.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment