Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba
BAADA ya Simba na Yanga kufungiwa kucheza kwenye uwanja wa Taifa wa Dar es salaam kwa kile kitendo cha uvunjifu wa viti uwanjani, Mabingwa watetezi wa Tanzania bara, Yanga wameuomba uongozi wa Chama cha Soka visiwani Zanzibar ‘ZFA’ kutaka kuutumia uwanja wa Amaan kuwa moja ya kiwanja chao katika mechi za ligi kuu zinazoendelea kutimua vumbi.
Taarifa zilitufikia ni kwamba ZFA, kimepokea kwa mikono miwili taarifa za klabu ya Yanga kumuandikia barua Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Zanzibar kuomba kuutumia uwanja wa Amaan kwa mashindano mbalimbali ambayo inashiriki ikiwemo ligi kuu Tanzania bara pamoja na mashindano mengine.
Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Zanzibar, afisa Habari wa ZFA Ali Bakar ‘Cheupe’ amethibitisha kuiona barua hiyo kupitia mitandao mbali mbali ambapo amesema wao kama ZFA hawana matatizo yoyote na wapo tayari hata baadhi ya michezo ya Ligi kuu Zanzibar kuisogeza hadi saa 12 jioni kuipisha Yanga au Yanga kucheza 12 jioni kupisha ligi kuu ya Zanzibar yote yanawezekana.
Amesema endapo Yanga wakikubaliwa kuutumia uwanja huo wa Amaa,  ZFA inaikaribisha Yanga visiwani Zanzibar.
“Bila shaka tumeziona  taarifa hizo kupitia mitandao mbali mbali, sisi ZFA tunathibitisha barua hiyo tumeiona, na  sisi kama chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar hatuna pingamizi juu ya klabu ya Yanga ambao ni sehemu ya Jamhuri ya Tanzania, sisi tunawambia karibu Zanzibar na tupo pamoja ikiwa watapata ridhaa huko walipoomba” Alisema Cheupe.
Barua hiyo ya Yanga iliyoandikwa na Katibu wao Baraka Deuedit imetumwa moja kwa moja kwa Waziri wenye dhamana katika wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Zanzibar huku nakala ikienda kwa Chama cha Soka Visiwani Zanzibar ‘ZFA’
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline




Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.