Halloween party ideas 2015
Image

Na Issa Ramadhan



MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma ya Nishati na Maji Tanzania, (EWURA), wametangaza bei mpya za kikomo za bidhaa za mafuta ya Petroli nchini kwa mwezi Oktoba ambazo zimepungua kulinganishwa na za mwezi uliopita.



Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWURA, amesema kuwa bidhaa za mafuta ya Petroli nchini kwa mwezi Oktoba ambazo zimepungua kulinganishwa na za mwezi uliopita.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa EWERU, Titus Kaguo amesema ni muhimu wauzaji wa mafuta wakatambua bei hizo mpya za kikomo ili kuepusha misuguano.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo imesema kuwa sababu kubwa ya kushuka kwa bei hizo za mafuta aina ya petrol, dizeli na mafuta ya taa inatoka na kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia.
Aidha ,Ewura imesema kuwa itaendeklea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta ikiwa na lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.
Bei za mafuta ya Petrol, Dizeli, na mafuta ya taa zimebadilika ikilinganishwa na tolea la tarehe 7 Septemba ambapo kwa mwezi Oktoba Bei ya petroli imepungua kwa shilingi 12 sawa na asilimia 0.66, dizeli kwa shilingi 48 sawa na asilimia 2.76 na mafuta ya taa kwa shilingi 15 sawa na asilimia 0.91.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.