Na Yusuph Mwamba
Rais Kabila, amesema hayo jana Ikulu Jijini Dar es Salaam, wakati wa dhifa wa kitafa iliyoandaliwa kwa ajili yake na Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 3 nchini Tanzania.
Rais Kabila amesema kuwa amani na umoja iliyopo nchini Tanzania ni ya kuigwa na wananchi wa nchi yake ili kuweza kufaidika na rasimali nyingi walizobarikiwa katika taifa hilo lenye mgogoro wa kivita na kisiasa kwa muda mrefu.
Aidha Rais Kabila amesema katika upande wa kibiashara nchi hizo mbili zimekuwa marafiki wa muda mrefu katika masuala hayo ambapo karibu asilimia zaidi ya 50 wanatumia bandari hiyo huku akiahidi kutumia zaidi bandari ya Dar es Salaam kama bandari rasmi ya kupitishia mizigo yake.
Kwa upande wake Rais wa Tanzania amesema atahakikisha kuendelea kudumisha ushirikiano na nchi hiyo katika nyanja zote kama ilivyokuwa katika utawala uliopita ili kujenga uchumi baina ya nchi hizo mbili.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment