Na Yusuph Mwamba
Moja ya Mashine za kutibu Kansa, lakini kwa sasa Tanzania itakuwa na mfumo wa simu wa kuwasilisha vipimo kwa kupiga picha kwenye simu. |
Uchunguzi na matibabu ya kansa ni utaalamu wa onkolojia ndani ya somo la tiba.Lakini kutokana na jitihada zinazofanywa na baadhi ya wataalamu wetu hivi karibuni wamegundua kifaaa ambacho kinawezakutumika kugundua Saratani hiyo
Watafiti wa Kaskazini mwa Tanzania wametengeza programu ambayo wauguzi na madaktari wanaweza kuitumia kuchunguza saratani ya kizazi miongoni mwa wanawake ,ambayo ni ya kwanza na ya kipekee duniani.
Program hiyo Inahitaji madaktari kupiga picha mfuko wa uzazi kwa simu janja (smartphone) na baadaye kutuma picha hiyo kwa kutumia programu hiyo kwa mtaalam wa matibabu katika kliniki maalum.
Daktari katika kliniki hiyo watachunguza picha hiyo na kutuma tiba kupitia program hiyo kwa mfanyakazi wa kiafya akitoa maelezo kuhusu tiba hiyo.
Ingawa kuna tatizo la mawasiliano ya simu, programu hiyo inaruhusu wafanyakazi hao wa kiafya kupiga picha hizo na kuzihifadhi kabla ya kuzituma baadaye.
Nchini Tanzania, zaidi ya wanawake 4,000 hufariki kila mwaka kutokana na saratani ya mfuko wa uzazi, kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment