Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba
KLABU ya Manchester United, i
mepokea kipigo cha mbwa mwizi dhidi ya timu ya soka ya Borussian Dortmund baada ya kufungwa kwa jumla ya magoli 4-1 katika ufunguzi wa kombe la Mataifa unaoshirikisha vilabu katika maandalizi ya mismu ya ligi mbali mbali Duniani.


Mchezo huo, umepigwa Nchini China Shanghai ijumaa ya leo ikiwa ni moja ya mechi ya ufunguzi wa kombe hilo.
Kipindi cha kwanza kilimalizika huku klabu ya soka ya Dortmund ikifanikiwa kwenda mapumziko ikiwa mbele ya mabao 2-0, mabayo yaliyowekwa kimyani na wanandinga Gonzalo Castro pamoja na Pierre-Emerick Aubameyang aliyeifungia timu yake bao hilo kwa   mkwaju wa penati.
Licha ya kupoteza mchezo huo , lakini kocha wa Man United,Jose Mourinho , hakuweza kuwajumuisha  wanandinga wawili kaitika ufunguzi wa michuano hiyo  akiwemo nahodha wa klabu hiyo,Wayne Rooney na unahodha wake kuchukuliwa  Antonio Valencia  ,huku  Mlinda malango wa kimataifa wa Hispainia David de Gea kufuatia mapumziko mafupi baada ya kumalizika kwa fainali ya michuano ya Euro 2016 iliyomalizika hivi karibuni nchini Ufaransa.
Kwa upande wa klabu aya Dortmund, pia hawakuweza kuwajumuisha nyota wake wapya waliosajiliwa msimu huu akiwemo  Mario Gotze aliyerejea kunako klabu hiyo na nyota wa zamani wa klabu ya Chelsea ,Andre Schurrle, na klabu ya Wolfsburg aliyetua leo kunako klabu hiyo kwa ada ya uhamisho wa Euro milioni 
Timu zote ziliweza kufanya mabadiliko, huko Meneja mpya wa Manchester United, Jose Mourinho, akijaribu kuwa anzisha  kipindi cha kwanza baadhi ya nyota wake kama  Ashley Young, Marcos Rojo, Marcus Rashford and Sergio Romero.
Hadi kipyenga cha mwisho kinamalizika . Klabu ya Dortmund ifanikiwa kuibuka mshindi kwa jumla ya magoli 4-1 katika mchezo uliochezwa uwanja wa Shangahi huko china.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia website

Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.