Na Yusuph Mwamba
KLABU ya Soka ya Simba, yenye makazi yake mtaa wa Msimbazi Kariakoo imemtamburisha rasmi Patrick Kahemele, kuwa katibu mpya wa wekundu hao wa Msimbazi,ambaye atakuwa mtendaji mkuu wa klabu hiyo katika uendeshaji wa timu na mipango mbalimbali ya klabu.
Kahemele, ambaye alishawahi kuitumikia klabu ya Azam FC kama katibu wa klabu hiyo baada ya kutemwa na nafasi yake kuchukuliwa na Sadi Kawemba, amesani kandarasi ya miaka 2 kuitumikia klabu hiyo kwa nafasi ya katibu ambapo kwa muda mrefu wekundu hao wa Msimbazi hawakuwa na katibu mkuu.
Patrick Kihemele akiwa na wanachama we Simba baada ya kutambulishwa rasmi kuwa katibu wa klabu hiyo jana |
Licha ya kuondoka klabu ya Azam, lakini Kahemele alikuwa ni mtu muhimu kunako klabu hiyo ya wana lamba lamba wa Jiji, ambako mafanikio mengi unayo yaona Azam FC, yaliletwa na kiongozi huyo ambaye ana taaluma nzuri juu ya uwendeshaji wa klabu.
Ujio wa Kahemele Msimbazi, unaifanya klabu hiyo kuwa na mtendaji wa timu badala yake kuwaacha kuwatumia viongozi walio kuwepo kama makatibu wa klabu ikiwemo Mwenyakiti wa Kamati ya Usajili , Zakaria Hans Pop pamoja na viongozi wengine kama Manara na Rais wa klabu hio Evans Eveva.
Miongoni mwa mambo aliyo waahidi wana Msimbazi baada ya kulamba dili hilo la kuitumikia klabu hiyo, amesema kwa sasa Simba watarajie ubingwa uliotoweka muda mrefu kwa misimu minne mfululizo, pia amewataka wana Simba wampe ushirikiano mzuri na kufanya klabu hiyo kutokuwa tegemezi kwa pesa za watu wachache na badala yake wajikite kuweka vitega uchumi vitakavyo isaidia klabu kujiendesha yenyewe.
" Klabu ya Simba wavumilivu sana kama utawafanyia mazuri na kama utaenda kinyume nao basi watakushukia kwahiyo nawaahidi nitakuwa nao pamoja katika kuijenga Simba mpya". Alisema Kahemela
Patrick Kihemele ( kuulia) akikabidhiwa moja ya zawadi |
Post a Comment