Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba

KLABU ya Young Africans mabingwa wa ligi kuu  VPL mara 26 na washindi wa kombe la shirikisho la Azam Federation Cup, wamefanikiwa kunasa saini ya Mwanandinga Obrey Chirwa anaekipiga kunako klabu ya Platinum FC ya nchini Zimbabwe.

Obrey, aliyesajiliwa kutoka klabu ya Platinum FC ya Zimbabwe, kwa ada ya dora za Kimarekani 120000 zaidi ya shilingi milioni 240 za Tanzania, alifanikiwa kumaliza msimu wa 2015/2016 wa ligi kuu ya Zimbabwe akiweka kimyani jumla ya mabao5 katika michezo 8 aliyowahi kucheza kunako klabu hiyo.

Mwanandinga huyo ni miongoni mwa wanandinga wanaounda kikosi cha timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 23 Nchini Zambia, pia miongoni mwa timu alizowahi kuzitumikia ikiwa pamoja na Platinum FC ni klabu ya Konkola Blades ya nchini Zambia.

Usajili huu, unaifanya klabu ya Dar Young Africans kutimiza jumla ya wanandinga 3 ndani ya klabu hiyo waliwahi  kuitumikia klabu ya Platinum FC ya Zimbabwe, miongoni mwa wanandinga hao ni Thaban Scala Kamusoko, Donald Dombo wote hawa ni raia wa Zimbabwe Ngoma na Obrey Chirwa raia wa Zambia.

Baada ya usajili huo, vyanzo nya habari vilifanikiwa kumtafuta kocha wa klabu hiyo  Hans Pluijm, ambaye alikili kuwepo na usajili huo na kusema kwa sasa hawezi kuzungumzia swala hilo na badala yake nguvu na akili akielekezea katika pambano la kesho la michuano ya shirikisho barani Afrika dhidi ya Mo bejaia.

Wakati nusajili ukiendelea kunako klabu hiyo, Yanga imefanikiwa kuwasili salama katika Jiji la Algeria tayari kushuka dimbani katika pambano lao dhidi ya wapinzani wao Mo Bejaia ya Algeria katika pambano linalotarajia kupigwa kaitika dimba la Unite Maghrebine Mjini Bejaia Algeria mishale ya saa 6 usiku kwa saa za Afrika Mashariki kwa kile kinachodaiwa kuwepo na mfungo wa mwezi wa ramadhani.

Katika mchezo huo wa Yanga didi ya Mo Bejaia,  mwamuzi wa kati anatikea Morocco, Bouchaub El Ahrach, akisaidiwa na waamuzi wa pembeni Redavane Achik pamoja na Youssef Mabrouk 

Yanga ilifanikiwa kufika kwtika hatua ya makundi ya fainali ya kombe la shirikisho baada ya kuwatoa wa Angola klabu ya Esparanca Sagrada kwa jumla ya mabao 2-1, ammbapo kwenye mchezo wa nyumbani Yanga iliibuka na usindi wa mabao 2-0 yaliyowekwa kimyani na wanandinga wake Saimon Msuva na Matheo Anthony baada ya mchezo wa marudiano uliofanyika Angola pamija na Yanga kufuzu makundi laikini ilijikuta ikipokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Sagrada ya Angola.

Baada ya mchezo huo dhidi ya Mo Bejai, klabu ya Yanga itarejea Dar es salaam kuwakabili mabingwa wa Afrika TP Mazembe ya DRC ya Congo juni 28 kwenye uwanja wa Taifa Dar es salaam.


Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.