Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba
MENEJA wa klabu ya soka ya JKT Ruvu na mtaalamu wa maswala ya mpira wa miguu King Abdallah Kibaden, ameweka wazi mipango yake ya kubaki kunako klabu hiyo kwa lengo la kuipa mafanikio zaidi.
Licha ya kuwatumikia maafande hao kwa sasa, lakini ameshapata kuvitumikia baadhi ya vilabu kongwe hapa Nchini ikiwemo Simba Sports Klabu na kufanikiwa kuiongoza klabu hiyo ya Msimbazi kufika katika hatua ya fainali ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika (CAF) mnamo mwaka 1993, na kukiongoza kikosi cha Moro United katika fainali ya michuano hiyo ya CECAFA Kagame Cup 2006 pamoja na timu ya Taifa, Taifa Stars miaka ya nyuma.
Kibadeni amesema kwamba, ataendelea kukinoa kikosi cha JKT Ruvu ya Pwani ambacho kilinusurika kushuka daraja katika msimu wa 2015/2016 ligi kuu bara uliomalizika mwaka huu.
“Nitaendelea kuwa kocha wa JKT Ruvu kwa sababu wao wenyewe wamniomba niendelee kuwa nao, pia katika ripoti yangu nimeona ni vitu gani vinahitajika kufanyiwa kazi ili mradi tusirudie makosa yaliyotupata msimu uliomalizika na kuona timu inashinda mataji nasio kupambana kwa ajili ya kutoshuka daraja.”Alisema Kibadeni
Wakati huo akieleza matarajio yake kwa maafande hao, pia ameuomba uongozi wa Jeshi hilo kutojenga makundi na kuwa na timu 6-7 za JKT haitakuwa na maana kwa sababu kitu kizuri huja baada ya kukaa pamoja badala yake kuwa kitu kimoja katika kuaanda timu ambayo itakuja kuleta upinzani mkubwa na kuweza kuzizima klabu kongwe hapa Nchini.

JKT Ruvu imefanikiwa kumaliza msimu wa 2015/2016 wa ligi kuu Tanzania Bara(VPL) kushika nafasi ya 11, ikiwa na jumla ya alama 32 nyuma ya Kagera Sugar yenyewe ikiwa imejikusanyia jumla ya alama 31 na kushika nafasi ya 12.













Kibadeni(kulia) akifuatilia moja ya mchezo VPL 2015/2016

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.