Amesema mfuko huo unalenga
kufanikisha ukusanyaji wa fedha za kutosha amabazo ni muhimu kwa Taifa
wakati huu tunapoazimia kumaliza ukimwi ifikapo mwaka 2030..
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo leo
(Jumanne, Novemba 28, 2017) wakati akifungua kongamano la Kitaifa la
maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani, lililofanyika jijini Dar es
Salaam.
“Nitoe wito kwa Bodi ya Mfuko huu
na watendaji wake kuhakikisha wanasimamia kikamilifu fedha hizi ili
ziweze kufanikisha malengo ya kuanzishwa kwa Mfuko huu. “
Waziri Mkuu amesema Serikali ya
Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli itaendelea kutenga fedha
za mfuko huo na kuhamasisha wananchi, wadau na sekta binafsi kuchangia
mfuko huo muhimu.
Wakati huo huo, Waziri Mkuu
amesema Serikali imedhamiria kujenga nchi ya viwanda ili waweze kufikia
uchumi wa kati, jambo ambalo haliwezi kufikiwa iwapo wananchi wake
watakuwa hawana afya bora.
“Hatutaweza kufikia malengo haya
kama Taifa iwapo watu wetu hawatakuwa na afya bora kwani nguvu kazi kwa
ajili ya Tanzania ya Viwanda itatokana na wananchi wenye nguvu na afya
bora.”
“ Hivyo kama Serikali
tutahakikisha tunaendelea kutoa huduma bora za afya ili wananchi wetu
waweze kuwa na afya bora. Tutaendelea kuwakinga wananchi wetu hususan ni
vijana ili Taifa letu liwe na nguvu kazi ya kutosha hasa wakati huu
tunapoanza mageuzi makubwa ya kiuchumi na kimaendeleo.”
Pia Waziri Mkuu amesema kwamba kwa
sasa Watanzania wengi wana uelewa mkubwa wa ukimwi lakini changamoto
iliyopo ni kubadili tabia na kuachana na tabia hatarishi zinazosababisha
kupata maambukizo mapya.
Amesema jambo hilo ni hatari kubwa
kwa nchi yetu kwa sababu bado wananchi wengi wanaendekeza tabia ya kuwa
na wapenzi wengi tena kwa wakati mmoja na hakuna uaminifu katika ndoa.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu “changia mfuko wa udhamini wa udhibiti ukimwi, okoa maisha”.
Kongamano hilo lilihudhuliwa na
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Walemavu Bibi Stella Ikupa
Alex, Naibu Waziri Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na
Watoto Dkt. Faustine Ndungulile, Makamishna wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi
Tanzania (TACAIDS).
Wengine ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dkt Leonard maboko,
Mwenyekiti wa Baraza la Wanaoishi na virusi vya Ukimwi (NACOPHA),
wawakilishi wa wadau wa maendeleo na wadau wa ukimwi nchini.
Post a Comment