Halloween party ideas 2015
Image


Na florah Raphael
MKURUGENZI wa tehama wizara ya ardhi,nyumba na Maendeleo na makazi amepewa miezi saba kukamilisha mradi wa mfumo unganishi wa taarifa za ardhi(ILMIS).
Ujenzi huo wa mfumo wa tehama katika wizara ya Ardhi unadhaminiwa na Benki ya Dunia ikishirikiana na kampuni ya IGN FI unategemewa kumalizika June 2018.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Dar es salaam Waziri wa Ardhi, Nyumba maendeleo na makazi William Lukuvi amesema kuwa serikali inaendelea kubadirisha mfumo wa kutunzia takwimu ili kupunguza ulasimu.
"Tunataka mfumo wa kutunza Kumbukumbu za ardhi huwe wa kisasa ili kupunguza wizi na uzalilishaji na lengo letu nikusambaza mfumo huu nchi nzima na kuongeza ufanisi katika kazi" amesema lukuvia
" Na 1juni 2018 tutazindua hati ya kidigitali ambayo taarifa zote zitakuwa zinapatikana kupitia mfumo hui kwani kutakuwa na uwezo wa kumtambua kila MTU ambaye ajalipa Kodi,kupunguza makanjanjana nani anayedaiwa kodi, pia serikali itaongeza kipato" ameongeza Lukuvi.
Aidha Shabani Pazi Mkurugenzi wa tehama Wizara ya ardhi,Nyumba maendeleo na makazi amesema dhumuni la mradi huu ni kuimarisha usalama katika umiliki wa ardhi  na kuboresha  usahihi wa manunuzi ya ardhi.
Vilevile Pazi amesema kuwa mradi huu umeanzia Kanda ya Dar eso salaam na manispaa ya kinondoni, mradi utahusisha usimamizi wa ardhi, usajili na upimaji, na kuhamisha taarifa za ardhi na Ramani katika mfumo wa kielektroniki.
Pia pazi amesema kuwa utatoa huduma za ardhi nafuu, usalama sahihi wa wateja, kuzuia uvamizi wa ardhi, misitu, na hifadhi ya barabara, kupunguza rushwa katika malipo, usajili na uhamishaji wa hati.
"Mfumo huu utamtambua kila MTU Mwenye hati na tutaongeza mapato kwa kiasi kikubwa, MTU akimiliki hati tutapunguza migogoro ya ardhi,kununua kuuza, kukodisha,ati itatumika kama dhamana ya mkopo Benki au taasisi za kifedha" amesema pazi.

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.