Na. Zephania. kapaya
Wakati tukishuhudia timu kongwe nchini za Simba na Yanga zikivutwa mashati nakuambulia pointi moja hali hiyo hiyo pia imekuwa sio nzuri kwa Azam ambao matarajio ya wapenzi wengi wa mpira nchini waliamini Azam angeipiku simba na kuongoza ligi, lakini wameshindwa kuiondoa Simba kwenye nafasi ya kwanza
kwenye msimamo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kubanwa na Mtibwa na
kulazimishwa sare ya kufungana 1-1 kwenye uwanja wa Azam Complex,
Chamazi.
Azam walitangulia kupata bao dakika ya 56 likifungwa na Enock Atta na
kutoa matumaini huenda Azam wangefanikiwa kuongoza ligi kwa tofauti ya
pointi mbili dhidi ya Simba endapo wangeshinda mchezo huo. Kelvin Sabato
aliyetokea benchi, akaisawazishia bao Mtibwa Sugar dakika ya 75 na
kuinyima Azam nafasi ya kukaa kileleni mwa ligi.Matokeo hayo yameifanya Azam kufikisha pointi 23 na kusalia katika nafasi ya pili licha ya kulingana kwa pointi na ‘mnyama’ lakini wastani wa magoli ndio unazitofautisha timu hizo katika nafasi ya kwanza na ya pili.
Timu zote za Dar (Yanga, Simba na Azam) zimeshindwa kupata matokeo ya ushindi kwenye mechi zao za raundi ya 11 baada ya kujikuta zikikaziwa na kulazimishwa sare ya kufungana 1-1 (Yanga 1-1 Tanzania Prisons, Simba 1-1 Lipuli na Azam 1-1 Mtibwa Sugar.
Post a Comment