Mkurugenzi
Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu (kulia), akizungumza na maofisa wa
Hospitali ya Rufaa ya Amana wakati wa ziara yake ya kikazi ya siku moja
Dar es Salaam leo ya kujua changamoto za upatikanaji wa dawa katika
hospitali hiyo na kuzitafutia ufumbuzi. Kushoto ni Mganga Mkuu wa
Hospitali ya Rufaa ya Amana, Meshack Shimwela.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Amana, Meshack Shimwela, akisisitiza jambo katika mkutano huo.
Maofisa wa Hospitali ya Rufaa ya Amana wakimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa MSD,Laurean Bwanakunu.
Meneja
wa MSD Kanda ya Dar es Salaam , Celestine Haule akichangia jambo wakaz8i
akizungumza na maofisa wa Hospitali ya Rufaa ya Amana.
Mfamasia wa Hospitali ya Rufaa ya Amana, Anna Kajiru (kulia), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
Mkurugenzi
Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu (wa sita kushoto), akiwa katika picha
ya pamoja na maofisa wa Hospitali ya Rufaa ya Amana.
Mkutano ukiendelea.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dk. Julius Mwaiselage akizungumza katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean
Bwanakunu akisisitiza jambo wakati akizungumza na maofisa wa Taasisi ya
Saratani ya Ocean Road katika ziara hiyo ya siku moja.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dk. Julius Mwaiselage ( kulia), akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu wakati wa ziara hiyo.
Mkurugenzi
Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu (wa tano kulia), akiwa katika picha ya
pamoja na maofisa wa Taasisi ya Saratani Ocean.
Na Dotto Mwaibale
TAASISI
ya Saratani ya Ocean Road wameipongeza Bohari ya Dawa (MSD), kwa
usambazaji wa dawa katika taasisi hiyo na maeneo mengine nchini.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dk. Julius Mwaiselage
wakati akizungumza na watendaji wa MSD ambao walifanya ziara ya kikazi
ya kujua changamoto mbalimbali za usambazaji dawa katika taasisi hiyo
wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu.
Katika
hatua nyingine upatikanaji wa dawa za saratani,vifaa tiba na
vitendanishi vya maabara katika taasisi hiyo ni asilimia 80 kutoka
asilimia nne mwaka 2015.
Kutokana
na hatua hiyo taasisi hiyo imesema ipo haja jamii kutambua mchango
mkubwa unaotolewa na Bohari ya Dawa MSD katika kupunguza changamoto za
huduma za saratani ambapo ilikuwa kero miaka miwili iliyopita.
Mwaiselage alisema hapo awali upatikanaji wa dawa vifaa tiba na vitendanishi ilikuwa ni changamoto kubwa katika utendaji.
“2015
taasisi hiyo ilikuwa ikipata dawa,vifaa tiba na vitendanishi asilimia
nne sasa ni asilimia 80 haya ni matokeo mazuri ya utendaji wa kazi wa
MSD,” alisema.
Alisema bajeti ya taasisi hiyo mwaka 2015 ilikuwa ni sh.milioni 790 na sasa ni sh.bilioni saba jambo ambalo linatia faraja.
Mkurugenzi
Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema taasisi hiyo inatambua kuwa
dawa za kansa ni gharama lakini atahakikisha zinaendelea kupatikana kwa
wakati ili kuokoa maisha ya watanzania.
Alisema suala la vifaa vya maabara ni tatizo linalohitaji mpango wa kitaifa wa manunuzi.
“Nawahakikishia
Ocean Road ni mteja muhimu hivyo nipo tayari muda wote kuwahudumia
leteni orodha ya mahitaji ya dharura hata leo,” alisema.
Mfamasia
wa Hospitali ya Rufaa ya Amana, Anna Kajiru alisema katika Hospitali
hiyo upatikanaji wa dawa kutoka MSD ni asilimia 80 na kuwa hali hiyo
imetokana na ushirikiano mzuri baina yao.
“Hivi
sasa hali ya upatikanaji wa dawa ambazo zinahitajika sana na wananchi ni
mkubwa mkubwa tofauti na zamani na hii inatokana na kazi nzuri
inayofanywa na ninyi MSD” alisema Kajiru.
Mkurugenzi wa MSD, Laurean
Bwanakunu na maofisa wake yupo katika ziara ya kikazi ya kutembelea
Hospitali za Mkoa wa Dar es Salaam ambapo leo alitembelea Hospitali ya
Rufaa ya Amana na Saratani ya Ocean Road na kesho atazitembelea
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Vijibweni na Temeke.
Post a Comment