Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Akizungumza kwenye Mkutano
Mkuu Maalumu wa Umoja wa Wanawake wa CCM Mkoa wa Mbeya uliofanyika
katika Ukumbi wa Shule ya Kutwa ya Mbeya, Jana Novemba 28, 2017.
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Akisakata rumba kwenye Mkutano
Mkuu Maalumu wa Umoja wa Wanawake wa CCM Mkoa wa Mbeya uliofanyika
katika Ukumbi wa Shule ya Kutwa ya Mbeya, Jana Novemba 28, 2017.
Makada wa CCM Mkoani Mbeya wakimlaki Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa Wakati akiondoka kwenye Mkutano

Na Mwandishi Wetu, Mbeya
Wajumbe
wa Jumuiya mbalimbali za Chama Cha Mapinduzi (CCM) wametakiwa kuchagua
viongozi waadilifu, weledi na wenye maono ya kuziongoza Jumuiya hizo ila
kuendana na kasi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akizungumza
wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Umoja wa Wanawake wa CCM Mkoa wa
Mbeya uliokuwa na Ajenda ya uchaguzi wa viongozi wa Jumuiya hiyo Mkoa na
Taifa, Mhe Mwanjelwa ambaye ni mjumbe Halmashauri kuu ya CCM Taifa,
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa aliwasisitiza wajumbe hao
kutochagua viongozi kwa matakwa ya urafiki na kujuana Bali kuchagua
viongozi wa kazi watakaoisaidia jumuiya kuendana na mtazamo mpya wa CCM
Mpya na Tanzania Mpya.
Mbali
na kuwashukuru makada hao kwa kumchagua kuwa Mbunge wa Viti Maalumu
Mkoa wa Mbeya jambo lililopelekea Mhe Rais John Pombe Magufuli kumteua
kuhudumu nafasi muhimu ya Kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Mhe
Mwanjelwa alisema kuwa serikali ya awamu ya tano ni ya kazi hivyo
uchaguzi huo ni vyema kumalizika kwa kuwapata viongozi wachapakazi.
“Tunaelekea
kwenye Mbeya Mpya, CCM Mpya, UWT Mpya na Tanzania Mpya hivyo msichague
viongozi kutokana na makundi au watakaoendeleza makundi baada ya
uchaguzi Bali chagueni viongozi shupavu na wachapakazi” Alikaririwa Mhe
Mwanjelwa
Mhe
Mwanjelwa (MNEC), alisema kuwa atafanya ziara katika maeneo mbalimbali
ya Mkoa wa Mbeya ili kuangalia jinsi utekelezaji wa ilani ya CCM
inavyotekelezwa.
Mkutano
huo Maalumu ulimalizika kwa salama hapo Jana Novemba 28, 2017 katika
Ukumbi wa Shule ya Sekondari Mbeya ambapo viongozi mbalimbali
walichaguliwa katika ngazi ya Mkoa na Taifa.
Post a Comment