Halloween party ideas 2015
Image

 

 Msimamizi wa Kongamano la Afya (TANZANIA HEALTH SUMMIT) Dk. Rebecca John(kushoto) pamoja na Rais wa Kongamano la Afya Dkt  Omary Chillo(wa katikati) wakati akizungumza na wanahabari kwenye ukumbi wa habari maelezo jijini Dar es salaam
                            Na Hellena Matale Dar es salaam
Zaidi  ya wadau  wa afya 500 wakiwemo wataalamu wa afya  kutoka ndani na nje ya nchi  wanatarajiwa kushiriki katika mkutano wa kitaifa wa afya unaotarajiwa kufanyika Novemba 14 hadi 15 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Rais wa Kongamano la Afya (TANZANIA HEALTH SUMMIT) Daktari  Omary Chillo ambapo amesema lengo la la mkutano huo ni kuchangia juhudi za serikali katika kuboresha afya kwa kujadiliana changamoto zinazoikabili sekta ya afya na kuishia na mapendekezo yanayoonyesha suluhisho ya majadiliano hayo.

Aidha Dk. Chillo amesema  mkutano wa mwaka huu utahusisha vipengele mbalimbali ikiwemo vikao vya kuathiriana vitakavyogusa mada za maendeleo ya huduma za afya,khotuba kutoka kwa wataalamu wazoefu wa afya na majadiliano katika vikundi.

Kwa upande wake msimamizi wa kongamano hilo Dk. Rebecca John ametoa wito kwa asasi za kiserikali na washiriki wote kushiriki katika kongamano hilo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta ya afya.

Kongamano hilo la Afya  ni la nne la kitaifa ambalo limebeba kauli mbiu isemayo Ni jinsi gani tunaweza kufikia malengo ya kuimarisha upatikanaji wa afya bora kwa kuunganisha tafiti za kisayansi,ubunifu na sera za afya.

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.