RC Makonda ataka wakina mama wajasiriamali wenye Viwanda vidogo kupatiwa Ardhi.
Na Yusuph Mwamba
RC MAKONDA amefungua Kongamano la kuhamasisha Wanawake kuwa Mahiri Kibiashara ambapo amesema *atahakikisha anaendelea kutengeneza Mazingira mazuri kwaajili ya wenye Viwanda Vidogovidogo kufanya Shuguli zao pasipo vikwazo.* Akizungumza na Mamia ya Wanawake Wajasiriamali katika Kangamano hilo lililoandaliwa na *Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania VoWET RC Makonda* amewahimiza *Wanawake Wajasiriamali kujituma na kuwa Wabunifu katika uzalishaji wa Bidhaa zao* ili ziweze kuvutia Soko la ndani na Nje ya Nchi.
Aidha, Rc Makondaa mesema Serikali inayowajibu wa kutengeneza Mazingira Bora ya Biashara ndio maana amekuwa akipambana kila mara kuhakikisha anaboresha Mazingira ikiwemo kuwatafutia Mkopo wa Riba nafuu kutoka NSSF ambapo amewasihi Wanawake hao kuchangamkia fursa hiyo ili kukuza Biashara zao.
RC Makonda amesema jitiada zake za kuwanyanyua wenye Viwanda Vidogo hazitokoma hadi pale atakapotimiza azma yake na Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Drk .Magufuli* inayohimiza Uchumi wa Viwanda ambapo ametoa Wito kwa Wanachi kuibeba na kuitekeleza kwa Vitendo dhana hiyo.
Hata hivyo amesema kuwa ana mpango wa kutoa eneo Kigamboni kwaajili ya Viwanda Vidogovidogo* ili kukuza uchumi wa Taifa na Familia.
"Nisingependa kuona mtu anaetafuta kipato kwa njia halali anasumbuliwa wakati wale Majizi wanakula starehe, ni lazima nitengeneze mazingira mazuri ya kuwawezesha ninyi Wafanyabiashara mfike mbali kiuchumi, sasa mimi naboresha mazungira kazi inabaki kuwa kwenu, mjitume" Alisema Makonda.
Kwa upande wake Rais wa Sauti ya Wanawake Wajasiriamali Tanzania VoWET Bi Maida Waziri amempongeza RC Makonda kwa kujitoa kwa Wajasiriamali na kueleza kuwa lengo lao ni kukuza kazi za kijasiriamali na sasa wanatarajia kujenga chuo cha ujasiriamali kwaajili ya kuwajengea uwezo Wajasiriamali.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment