Daktari bingwa wa masikio, koo na pua, Jonas Ndasika ameshindwa kufanya upasuaji kutokana na ukosefu wa vifaa hivyo katika Hospitali ya Rufaa ya Ligula mkoani Mtwara.
Akizungumza baada ya kumaliza utoaji wa huduma za madaktari bingwa ulioandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Mganga Mfawidhi wa Ligula, Kariamel Wandi amesema utoaji wa huduma hizo umeonekana wa kusua sua kutokana na baadhi ya vifaa kukosekana na katika hospital hiyo.
“Daktari bingwa wa masikio, koo na pua ndiyo daktari pekee ambaye ameshindwa kufanya upasuaji kwa sababu hospitali yetu ya Ligula haina vifaa hivyo,” amesema.
“Vifaa vya masikio, koo na pua hakuna kabisa katika hospitali yetu na huduma hii haijawahi kutolewa kama iliwahi kutolewa labda miaka ya nyuma.”
Mganga huyo ameomba Serikali kuhakikisha hospitali ambazo zipo pembezoni zinakuwa na vifaa pamoja na madaktari ili kuweza kufanya kazi wa ufanisi mzuri zaidi.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment