DIWANI wa
kata ya Makurumla iliyoko Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, Omary Kambo, amewataka
dereva wa boda boda wote wahakikishe swala la ulinzi na usalama wanalisimamia
ipasvyo kwani matukio mengi yanahisihwa na na boa boda.
Akizungumza
na Gazeti la Raia Tanzania jana , Diwani Omary, alisema kumekuwa na matukio ya uporaji kata ya Makurumla yanayohusishwa na boda boda pamoja na Vishandu (waporaji) .
Aidha
aliwataka dereva wote wa boda boda kuwa makini na wale wanaotaka kuanzisha vijiwe
upya kwani wana vijiwe 19 wasikubali
vingine kuanzishwa endapo watabainika watafikishwa moja kwa moja kwenye vyombo vya sheria.
Akizungumzia
kukamatwa hovyo kwa boda boda, ,alisema
kuwa Jeshi la Polisi haliwakamati watu wasio na makosa hivyo aliwaomba wasikubali
kukamatwa na makosa wahakikishe wanazingatia sheria.
“Sheria zipo, na Jeshi la polisi linawajibika
kwa ajili ya usalama wenu, kama mtua atakamatwa basi atakuwa na kosa
hakikisheni mnakuwa salama muda wowote ili kuepukana na makosa hayo”alisema
Diwani
Hata hivyo ,
kwa upande wa Kaimu OCD Magomeni, Egfred Pius Kasikana , aliwataka boda boda
wote kuzingatia sheria na kutoa dhana ya kuweka uadui na Jeshi la Polisi kwani
wao wapo kwa ajili yao na kuwachukulia kama rafiki zao.
“Nawaombeni
Boda boda msiwaogope Polisi, tengenezeni urafiki nao, kama unamakosa mwambie
akwambie kosa lako ili usirudie tena kuliko kutoa rushwa jambo ambalo
litakufanya uwe muathirika wa rushwa na kuwanufaisha watu”aliongeza Egfred
Kuhusiana na
swala la tozo za leseni, Afisa Mtendaji wa kata ya Makurumla ,Muslima Mwenda ,
alisema kwa sasa boda boda wanatakiwa kukata leseni ya maegesho Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, tozo hizo
zimegawanyika sehemu mbili ambapo kwa tozo za leseni ni 22000 wakati 36000 ni kwa ajili ya tozo za maegesho .
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment