Na Mwandishi wetu, Dar
KLABU ya Ndanda FC ya mkoani Mtwara leo imeingia mkataba wa mwaka mmoja na kampuni ya Motisun Group kupitia kwa bidhaa yao ya Kiboko.
Hiyo ikiwa ni siku chache lanka ya Ligi Kuu Bara ianze kutimua vumbi Agosti 26, mwaka.
Akizungumza na jijini Dar, Mshauri wa
Masoko na Biashara wa Ndanda, Peter Simon alisema wanaushukuru udhamini
huo ambao utawasaidia wao kupambana na mikikimikiki ya ligi kuu kwenye
msimu ujao ambao anaamini utakuwepo mkubwa.
Simon alisema, udhamini utawawezesha wao
timu yao kusafiri nje ya mikoa kwa ajili mechi za ugenini huku
wakiahidi kutowaangusha kwa kipindi hicho cha mwaka mmoja.
"Niwaahidi Motisun Group kupitia kwa bidhaa yao ya Kiboko kuwatangaza vema kupitia timu yao itakayoshiriki ligi kuu.
"Ndanda tunaamini kuwa kupitia timu yetu wataongeza idadi ya wateja kutokana kuwatangaza vema, "alisema Simon.
Kwa upande wa Motisun kupitia kwa Mkuu
wa Masoko, Edward Mlyansi alisema kuwa "Kwa kuanza wanaanza na udhamini
huo wa mwaka mmoja na baadaye watauboresha zaidi hapo baadaye.
"Kikubwa wanataka kuona timu ikipata
matokeo mazuri na kuleta ushindani mkubwa na hatutaki kuona migogoro
katika timu, "alisema Mlyansi.
IUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline .
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline .
Post a Comment