Halloween party ideas 2015
Image



Na Mwanaid Mziray (Tsj) Dar es salaam
 
AFISA  Kitengo cha Chakula ,maji salama na mazingira kutoka Wizara ya afya, jamii, wazee, jinsia na watoto,Stephen Kiberiti, ameishauri jamii kuwa makini juu ya uhifadhi wa vyakula na kuepuka kutumia  mifuko ya plastiki kuhifadhi chakula.
Akizungumza nagazeti hili ofisini kwake,Kiberiti alisema anaishauri jamii kuhakikisha maeneo ambayo yanauzwa chakula ni safi na salama kwa afya, ikiwa ni pamoja na kuhifadhi chakula katika mazingira yanayo hitajika. 

“Nawashauri wanajamii wawe makini juu ya kuhifadhi vyakula na mazingira katika hali ya usafi na usalama kwa matumizi na afya kwa ujumla,”alisema Kiberiti
Aidha aliongeza kusema kwa kuitaka jamii kuhifadhi  vyakula katika mazingira yanayohitajika ili kuepukana na magonjwa hatarishi yenye kuambukiza kama vile homa za matumbo,kipindupindu na kuharisha.

Licha ya hivyo aliwaomba viongozi wa halmashari kuendelea kutumia sheria ndogo ndogo ili kudhibiti uchafuzi wa mazingira na kutoa elimu kwa jamii juu ya athari zitokanazo na mazingira kuwa machafu na namna ya kuepukana nayo kwa usalama wa afya zao.

“Hii sio kwamba tunawakatili wananchi ni kwajili ya kuweza kuona namna ya kuondokana na magonjwa hatarishi yasiyo ya lazima yanayoweza kuepukika,” alisema Kiberiti.

 IUNGE NASI , BONYEZA  HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, 
insta@wabunifumediaonline
.

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.