Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba

WAKATI  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt, John Magufuli akitoa ruhusa kwa wwafanya biashara wadogo wadogo maarufu kama Wamachinga kufanya shughuri zao huru pasi na kuingiliwa na mtu yeyote.

Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kesho anatarajia kukutana na wafanyabiashara hao ili kujua sababu ya kutokuwa tayari kwenda katika maeneo waliyopangiwa.

Makonda alisema lengo la kukutana na wafanyabiashara hao ni kujua kwa nini hawapo tayari kwenda katika maeneo waliyotengewa na kuangalia namna bora ya wao kufanya biashara zao ili kuondoa usumbufu uliopo sasa.

“Nitakutana na wamachinga katika mkoa wangu, nikiambatana na Wakuu wa Wilaya ili niweze kujua ni kitu gani kinachowafanya wao kushindwa kwenda katika maeneo yaliyotengwa. ”

Aidha, Makonda alisema hawezi kuruhusu utaratibu unaofanywa na machinga hao, ambao baada ya kauli ya rais wamerejea na kuweka biashara zao hata sehemu za watembea kwa miguu na kusababisha kero.

“Siwezi kuruhusu utaratibu uliopo sasa, wamefikia hatua ya kuziba barabara hata magari yanashindwa kupita wananchi wanapata taabu, nitakwenda kuonana nao na nitawasikiliza na baada ya kuwasikiliza tutakuja na uamuzi,” aliongeza Makonda.

Juzi Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ilisema inajiandaa kuanzisha Sabasaba Bonanza ili watu wasio na maeneo ya kufanya biashara, wakiwemo machinga, kutumia Viwanja vya Maonesho ya Biashara vya Mwalimu J. K Nyerere maarufu Sabasaba, kufanya biashara zao.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.