Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba 
CHELSEA  wamepigwa faini ya £100,000 na Manchester City wakapigwa faini ya £35,000 baada ya wachezaji wao kuhusika katika vurugu uwanjani wakati wa mechi ya Ligi ya Premia. 

Hisia zilipanda na wachezaji wakakabiliana mechi hiyo iliyochezewa uwanjani Etihad ilipokaribia kumalizika baada ya Sergio Aguero wa City kufukuzwa uwanjani kwa kumchezea visivyo beki wa Chelsea David Luiz.

Fernandinho pia alifukuzwa uwanjani kwa kumkaba koo Cesc Fabregas wachezaji wa klabu hizo mbili walipokabiliana baada ya kisa hicho.
Chelsea walishinda 3-1.
Blues walikuwa awali wametahadharishwa kwamba wanaweza kupokonywa alama kwa utovu wa nidhamu.
Viongozi hao wa Ligi ya Premia wamepigwa faini mara sita tangu Februari 2015 kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.