Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba 

WAKATI mtafaruku ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) ukiwa bado ni kizungukuti, jina la Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa likitajwa kuwa katikati ya mgogoro unaoendelea ndani ya CUF, mwanasiasa huyo ameibuka na kusema shida za chama hicho ni za Ukawa.

Tangu mgogoro huo uibuke baada ya Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba kujiuzulu nafasi hiyo na baada ya miezi 10 kurejea akitaka kuchukua nafasi yake, jina la Lowassa limekuwa likitajwa kuwa sababu ya kila hatua.

Profesa Lipumba alipojiuzulu alimtaja Lowassa kuwa kujiunga kwake Chadema na baadaye kupitishwa kuwa mgombea urais wa chama hicho na Ukawa, ndiyo sababu ya yeye kuachia ngazi katikati ya kampeni na hata aliporejea na kuibuka mgogoro, ameendelea kulitaja jina hilo kama sababu.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.