Na Yusuph Mwamba
UONGOZI wa aliyekuwa mgombea urais
wa chama cha Democratic Hillary Clinton dhidi ya Donald Trump wa
Republican katika kura za kawaida umeongezeka hadi kura milioni mbili.
Rais
Mteule Bw Trump alishinda uchaguzi huo wa urais uliofanyika tarehe 8
Novemba kwa wingi wa kura za wajumbe na ataapishwa Januari.Lakini kura za kawaida zinaendelea kuhesabiwa, wiki mbili baadaye, na kura za Cook Political Report zinaonesha ana kura 62.2m naye Bi Clinton 64.2m.
Hii ni mara ya tano kwa mgombea kuongoza kwa kura za kawaida lakini akashindwa uchaguzini kwani kura za wajumbe ndizo hutumiwa kuamua mshindi.
Mwaka 2000, mgombea wa Democratic Al Gore aliongoza dhidi ya George W Bush kwa karibu kura 544,000.
Baada ya mvutano wa muda mrefu mahakamani, Mahakama ya Juu mwishowe iliamua mshindi wa urais baada ya kumkabidhi Bw Bush ushindi katika jimbo la kushindaniwa la Florida.
Mwaka huu, Bi Clinton alipata kura nyingi katika majimbo kama vile California lakini Bw Trump alishinda majimbo ya kushindaniwa, na kupata kura nyingi za wajumbe.
Mfumo wa kura za wajumbe humfaa zaidi mgombea ambaye anashinda, hata kama kwa kura chache, katika majimbo mengine dhidi ya yule anayeshinda kwa kura nyingi katika majimbo machache.
- Melania Trump kuchelewa kuingia White House
- Clinton: Nilitaka kujificha kabisa
- Hillary: Trump apewe fursa ya kuongoza
- Wafuasi wa Trump wakerwa na uamuzi kuhusu Clinton
Wanashangaa ni kwa nini Bi Clinton alionekana kutofanya vyema katika wilaya zilizotumia kompyuta kupiga na kuhesabu kura ikilinganishwa na maeneoa mbayo watu walipiga kura halisi za karatasi na mitambo ya skana ya kuhesabu kura.
Lakini maafisa wa kampeni wa Clinton hawajaonyesha nia yoyote ya kutaka kura zihesabiwe tena.
Mgombea wa chama cha Green Party, Jill Stein, anachangisha pesa za kupigania kura zihesabiwe upya katika majimbo hayo ya Michigan, Wisconsin na Pennsylvania ambayo Bw Trump alishinda.
Hayo yakijiri Donald Trump kwenye hotuba yake Siku ya Kutoa Shukrani amewahimiza raia wa Marekani kuunga mkono juhudi zake za "kujenga upya nchi" na kuponya makovu baada ya uchaguzi uliokuwa na ushindani mkali.
Jumatano, Bw Trump aliwateua watu wengine wawili wa kuhudumu kwenye serikali yake, Nikki Haley kuwa balozi wa Marekani UN na Betsy DeVos kuwa waziri wa elimu.
Jinsi Donald Trump alivyoshinda urais
Kura za Donald Trump kwenye ramani
Republican
Kura za Hillary Clinton kwenye ramani
Democratic
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment