TIMU ya Majimaji kutoka Songea maarufu" wanawalizombe" wako jijini Dar es Salaam, tayari kwa mechi na kuivaa Simba Jumamosi mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa.
Pamoja na kuonekana kusua kwa kiwango katika mechi zote za mwanzo, Majimaji wanaonekana wamepania na wamejipanga kwa dhati kupata ushindi kwa kuifunga Simba na kupata pointi tatu muhimu.
Wamepolekewa vizuri na wadau na wapenzi wa timu yao mbalimbali ambao wangependa Simba ishindwe na kupewa huduma bora kabisa.
Majimaji wamefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana, hali inayoonyesha kuwa wana maandalizi makini na wako tayari kwa mtanange huo hasa.
Kama hiyo haitoshi, wamekamilisha mipango yao ya kumrejesha kocha wao wa zamani, Kali Ongala.
Ongala ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Abajalo kutoka timu ya Sinza na Yanga, aliondoka baada ya kuiwezesha kubaki Ligi Kuu Bara msimu huu.
Lakini taarifa kutoka ndani ya Majimaji, dhimethibitisha kurejea kwa kwa kocha huyo, huku akitarajia kuanza kuonekana kwenye benchi la ufundi la timu hiyo ya majimaji kwenye mchezo wao dhidi ya Simba unaotarajiwa kutimua vumbi siku ya Jumamosi.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment