Halloween party ideas 2015
Image


Na Issa Ramadhani,

SHIRIKI la afya ulimwenguni WHO, leo limezindua mkakati wa kukabiliana na magonjwa ya moyo yakiwemo shambulio la moyo na kiharusi, magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo duniani.

Kwa mujibu wa WHO, zaidi ya watu milioni 17 hufariki dunia kila mwaka kutokana na magonjwa ya moyo, wengi wa wanaofariki hugundulika kutumia tumbaku, kula vyakula vyenye chumvi nyingi, na kutofanya mazoezi.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Margaret Chan

Shirika hilo limesema wengi wanaweza kuokolewa kwa kupatiwa tiba za shinikizo la damu, shinikizo la lehemu na mengine yanayosababisha magonjwa ya moyo na kiharusi.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dkt. Margaret Chan, amenukuliwa akisema mkakati huo utaokoa maisha ya mamilioni ya watu kwa hatua za kuzuia magonjwa ya moyo katika jamii na katika nchi ikiwamo kuweka ushuru katika tumbaku, kupunguza vyakula vyenye chumvi na tiba mujarabu.

Mkakati huo ni sehemu ya jitihada mpya ya kuongeza kinga na udhibiti wa magonjwa ya moyo hususani katika nchi zinazoendelea, ambapo kituo cha Marekani cha udhibiti wa magonjwa na kinga US CDC ma wadau wengine wa afya wanajumuishwa.



JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline


Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.