Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba


MENEJA wa zamani wa klabu ya soka ya Manchester United na klabu ya soka ya Everton ,David Moyes, amekabidhiwa rasmi mikoba ya kufundisha klabu ya soka Sunderland.



Hatua hiyo imekuja kufuatia aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya soka ya Sunderland,Sam Allardyce , kuachia ngazi kunako klabu hiyo baada ya kuteuliwa kuiongoza timu ya Taifa ya Uingereza.



Kocha wa Uingereza, Roy Hugdso, alijiondoa kunako Taifa hilo kufuatia kufanya vibaya katika michuano ya Fainali ya Euro 2016 iliyomalizika hivi karibuni Nchini Ufaransa huku tukishuhudia wenyeji wa maandalizi hayo, Timu ya Taifa ya Ufaransa wakiambulia kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Ureno katika fainali hiyo iliyochezwa Julai 10, 2016 Ufaransa.

Siku alizo dumu kaika kukinoa kikosi cha Red Devil ni miezi 10 na alijiunga kunako klabu hiyo 1 Julai  2013, huku akifanikiwa kufikisha jumla ya michezo 513 akiwa kocha wa Everto ambapo alijiunga 14 Machi 2002 na kufanikiwa kukaa siku 364 alipojiunga Novemba 10, 2014 Novemba 9, 2015 kaika klabu ya soka ya Real Sociedad ya Nchini Hispainia huku akifanikiwa kuifundisha timu ya klabu ya Prestoni12 Januari 1998.



Michezo aliyocheza timu zote ikiwemo Preston amecheza jumla ya michezo 234, kushinda michezo 113, huku akipoteza michezo 63 huku akijinyakulia alama 48.29% za ushindi

Akiwa na klabu ya Everton, amecheza jumla ya michezo 513, huku akishinda michezo 216 na kupoteza michezo 159 huku akijinyakulia alama 42.11% za ushindi

Akiwa klabu ya Manchester United, alicheza michezo 51 na kushinda jumla ya michezon 27 huku akipoteza michezo 15 akipewa alama ya 52.94% za ushindi.




Akiwa klabu ya Real Sociedad amecheza michezo 42, huku akishinda jumla ya michezo 12, wakati huo akipoteza michezo 15 anapewa alama 28.57% za ushindi

Kwahiyo basi, licha ya taarifa zote zilizo orodheshwa hapo juu, kwa ujumla kocha, David Moyes, amecheza jumla ya michezo 840, huku akishinda jumla ya michezo 368 na kupoteza jumla ya michezo 252 na kujikusanyia alama 43.8 % za ushindi.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia website


Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.