TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA JUNI 25, 2016
Na Yusuph Mwamba
Klabu ya Manchester City ipo mbioni kuwania saini ya mshambuliaji wa kimataifa wa Hispaini anaye kipiga kunako klabu ya Celta Vigo ya Hispania Nalito, kwa dau la pauni milioni 13.8 kwenye majira ya usajili, wakati huo huo nayo klabu ya New Castle United ipo kwenye mawindo ya kuwania saini ya nyota wa Marseille ya Ufaransa Frolian Thauvin, kwa dau la pauni milioni 14 huku Marseille wakitaka dau hilo liongezwe hadi kufikia pauni milioni 18.
Naye nyota wa kimataifa wa Brazil anayekipiga kunako klabu ya Barcelona Neymar amesaini dili jipya kwenye klabu yake ya Barcelona lenye thamani ya pauni milioni 230, litakalo muwezesha kudumu Nou Camp mpaka kufikia mwaka 2022, wakati nyota huyo akiongeza dili hilo la kutumikia Barcelona msimu ujao kwa sasa Neymar JR, yupo Nchini Brazil katika Jiji la Rio De Janeiro kwa mapumziko.
Meneja mpya wa Manchester United, Jose Morinho, amesema bado haja kata tamaa ya kumwania nyota bwa kimataifa wa Italia, Poul Pogba ambaye anatumikia Taifa lakje kwenye fainali ya michuano ya Euro 2016 kwa dau la pauni milioni 97, lakini dili hilo huenda lisifanikiwe kirahisi kutokana na nyota huyo kuwindwa na vilabu mbalimbali ikiwemo Matajiri wa Dunia klabu ya Real Madrid ambayo iinaonekana kuvutiwa na nyota huyo, licha ya ushindani huo, Morinho amesema atatumia kisi chochchote cha pesa ili kuweza kumshawishi nyota huyo kujiunga na United katika msimu huu wa usajili.
Klabu ya Barcelona inawania saini ya nyota wa klabu ya Lyon Samuel Umtiti,kwa dau la pauni milioni 32, huku Arsenal ikionekana kuvutiwa na winga wa kimataifa wa Croatia, na klabu ya Inter Milan, Ivan Perisic wakati huo klabu ya soka ya Real Madrid ipo mbioni kuwania huduma ya nyota wa kimataifa wa Brazil , Gabriel Jesus, lakini ushindani wa kumpata nyota huyo unaonekana kuwa mkubwa huku baadhi ya vilabu vikubwa vikionesha nia ya kumtaka mwnandinga huyo ikiwemo Juventus, Man City na Barcelona lakini kama nyota huyo atakubali kujiunga na moja ya vilabu hapo juu watawajibika kulipa ada ya pauni milioni 24 kama uhamisho wake.
Nyota wa klabu ya Atletico Madrid, Oliver Torres, yupo mbioni kuondoka kunako klabu hiyo kwa kile kinchosemekana kutoendana na mfumo wa kocha Diego Simeon, nyota huyo mwenye umri wa miaka 21, amesema ni bora akatafute timu nyengine ambayo atapata nafasi ya kucheza kuliko kubaki kunako klabu hiyo, Lakini mwanandinga huyo mpaka sasa tayari ameshapata ofa mbalimbali ikiwemo vilabu vya Hispania, Uingereza na Ujerumani
Post a Comment