Na Yusuph Mwmba
MIGOGORO ya Ardhi imeendelea kuwa gonjwa sugu kwa wananchi wasiojiweza licha ya serikali kuhaidi kuendelea kuitatua na kushughulikia.
Hali hii imetokea jana ambapo, Wakazi wa kijiji cha Kilosa kata ya Mvuni iliyoko wilaya ya Kilosa, Mkoani Morogoro wakishirikiana na Viongozi wao wa kata, wamemuomba waziri wa ardhi, nyumba na makazi ,William Lukuvi, kuingilia kati mgogoro wa ardhi kati yao na mwekezaji ambaye anadaiwa kufanya dhulma ya Hekari zaidi ya 2180 Wilayani humo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mvumi ,Abdu Tumbo, amesema kuwa ni mgogoro wa muda mrefu ambao umekuwa sugu katika kijiji hicho ambapo muwekezaji amekuwa akinyanyasa wananchi wenye haki ya maeneo yao.
Mwenyekiti wa kata ya Mvumi, Abdully Tumbo, akijaribu kueleza jambo mbele ya wanakijiji katika saka la uporaji wa ardhi dhidi ya kigogo Wilayani hapo. |
Tumbo ameeleza kuwa, Eneo la Muwekezaji huyo anayefahamika kwa jina la Pateli ni ekali 524 ambazo ameweka wafugaji lakini sasa amekuwa akizidi kuchukua mashamba ya watu wengine na kuweka wakulima na kukodisha mashamba ya watu waishio Wilayani humo.
Wanakijiji cha Mvumi Wilayani Morogoro kata ya Mvumi Mkoa wa Morogoro wakiwa ndani ya eneo linalodaiwa kuporwa na kigogo. |
Kwa upande wa Mfugaji Kidanyenye Kidasaki, amesema kuwa wanaomuomba Waziri Lukuvi aende eneo hilo ili kutatua kero hiyo ya muda nmrefu kwani wafugaji katika eneo hilo wamekuwa wakinyanyaswa na kufukuzwa pia kuhamisha mara kwa mara mpaka mifugo yao inakufa bila hatia kwa sababu ya kuhama.
Baadhi ya wafugaji na Wanakijiji cha Mvumi wakitembelea eneo linalodaiwa kuporwa na kigogo Wilayani humo |
Aliongeza kuwa kuwa kila mwezi muwekezaji Patelianakuja kuchukua laki 4 kwa sababu ya wao kutumia eneo hilo ambalo sio lake.Kabushi Mateu ambaye ni Mkulima, amesema kuwa wakulima wamekuwa wakinyanyasika na hali ya uchumi ilivyokuwa ngumu kwani wamekuwa wakipangiwa fedha kubwa katika kukodi eneo la kulima, ambapo Naibu Katibu mkuu wa kikundi cha wakulima kijiji cha Mvumi, Asha Kurususu ,amesema kuwa hali ya kiuchumi kwao inazidi kuwa mbaya kila uchwao ni vyema mamlaka husika zikalitatutua hilo kwa ustawi wa wananchi wake.
Post a Comment