MABINGWA wa Ligi kuu Uingereza msimu wa mwaka 2015/2016, Klabu ya Leicer City, imezima rasmi ndoto za Mwanandinga wake Jamie Vardy kutua kunako klabu ya Arsenal katika dirisha la usajili msimu huu.
Vard, ambaye alifanikiwa kumaliza msimu wa mwaka 2015/2016 vizuri baada ya kufanikiwa kufumania nyavu mara 24, na kuibuka mfungaji bora katika ligi kuu ya Uingereza.
Kauli hiyo imekuja muda mfupi baada ya Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Leicer City, Aiyawatt Srivadhanaprabha,kutangaza dau jipya la mshahara wa mwanandinga huyo kitka kikosi cha klabu hiyo msimu ujao.
Arsenal ilitoa ofa ya Mwanandinga huyo kwa dau la pauni milioni 20, na kutaka kumlipa mshaara wa pauni 100,000 kwa wiki kabla ya mwanandinga huyo kuitumikia timu yake ya Taifa ya Uingereza katika fainali ya michuano ya Euro2016, lakini Vardy alichelewa kutoa maamuzi mapema mpaka michuano hiyo inaanza.
Kwa sasa klabu yake imempandishia mshahara mwanandinga huyo hadi kufikia kiasi cha pauni 100,000 sawa na kile walichotaka kulipa klabu ya Arsenal endapo angesaini kunako klabu hiyo ya Washika bunduki wa London.
"Vardy ni mchezaji wetu, amefanya mengi sana nmpaka tunafanikiwa kutwaa ndoo ya Uingereza amechangia kwa kiasi kikubwa, lakini ndoto zetu ni kumbaisha kunako klabu yetu kwa ajili ya msimu ujao ikiwemo mashindano ya kombe la mabingwa barani ulaya (UEFA), tunahitaji kuwa na kikosi bora ili kujenga timu imara na yenye ushindani". Alisema Aiyawatt
Jamie Vardy akishangilia bao lake katika moja ya mechi ligi kuu Ungereza msimu wa 2015/2016 |
Post a Comment