Na Shariff Shabani
Ukosefu wa hofu ya mungu,upendo na umoja zimetajwa kuwa sababu kubwa zinayosababisha mauaji na vitendo viovu hadi katika nyumba za ibada.
Ni maneno yaliyosemwa leo katika mkutano mkuu wa sinodi ya 19 uliofanyika jijini Dar es salaam na Mhashamu Askofu Dokta Valentino Mokiwa wa kanisa kuu la Albano Mtakatifu ikiwa ni siku chache tu toka kuuwawa kwa watu saba ndani ya msikiti jijini mwanza.
Mhasham Askofu alisema kuwa mbali na watu wa kawaida kutokuwa na hofu ya mungu hata watumishi wa mungu pia hawana hofu ya mungu hali inayofanya hata waumini kutokuwa na imani naviongozi wao wa dini.
Aidha Mokiwa alisema kuwa kanisa la anglikana linakabiliwa na changamoto ya kuhujumiana na kufanyiana mambo yasiyowawakilisha vizuri kwa watazamaji wanaoamini kwamba hilo ni kanisa lenye kuamainika na kuheshimika.
"Tunahitaji kuwa na kanisa lililisimama vizuri lenye mafundisho imara ,safi na mazuri.kanisa lenye kuvutia wengi kwa sera,maono,ibada na misimamo " Alisema Mokiwa.
Mbali na kuwa na changamoto zinazolikumba kanisa hilo kanisa limefanikisha kufanya upanuzi wa hospitali iliyopo Buguruni,maboresho ya huduma,ujenzi wa maabara ujenzi wa chumba cha upasuaji pamoja na kuanzishwa kwa huduma za HIV ambazo huwa na wagonjwa zaidi ya 2000.
Kwa upande wake Father Jonson Lameck wa kanisa hilo aliwaasa watu wawe na mioyo ya imani na kumuheshimu mungu.
Post a Comment